Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Tovuti Iliyonisaidia Kutengeneza Milioni 20 Mtandaoni

Sehemu ya mwisho jinsi nilivyo tengeneza milioni 20 mtandaoni
Tovuti Iliyonisaidia Kutengeneza Milioni 20 Mtandaoni Tovuti Iliyonisaidia Kutengeneza Milioni 20 Mtandaoni

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao umefuatiia makala hii tokea mwanzo basi lazima utakua unajua kuhusu sehemu hii ya mwisho, sehemu hii ni mwendelezo wa sehemu mbili zilizopita ambapo nilishare na nyie jinsi nilivyoweza kubadilisha maisha yangu kwa kutengeneza pesa mtandaoni zaidi ya milioni 20.

Kama ulipitwa na makala hizo unaweza kusoma hapa kuangalia sehemu ya kwanza ya makala hii, na pia unaweza kusoma hapa kuangalia sehemu ya pili ya makala hii. Sehemu ya tatu leo nitamalizia siku ya leo na kuonyesha tovuti yenyewe iliyo nisaidia kutengeneza pesa. Kwa kuanza nivizuri kuangalia video hii hapo chini kisha endelea kwenye maelezo hapo chini.

Advertisement

Kubadilisha Rangi

Kama unataka kubadilisha rangi, bofya sehemu ya Theme Settings, kisha bofya sehemu ya rangi iliyopo kulia na chagua rangi unayotaka. Chagua rangi ambazo zinakaribia kufanana kwenye chumba cha juu na cha chini au unaweza kuchagua rangi zinazo fanana kidogo. Baada ya hapo bofya kitufe cha Save Theme.

Tovuti Iliyonisaidia Kutengeneza Milioni 20 Mtandaoni

NOTE : Baada ya ku-save utaona rangi bado hipo hiyo hiyo hii inatokana na cache ambayo inahifadhiwa kwa simu moja ama mbili, so utaona rangi imebadilika kama ukitumia kifaa kingine kuangalia tovuti yako. Rangi itabadilika kwenye kifaa ulicho tumia baada ya siku moja.

Ili kubadilisha Logo unatakiwa kuwa na logo za aina mbili, unatakiwa kuwa na logo isitozidi upana wa 200 na urefu wa 44 (200 x 44px). Pia unatakiwa kuwa na Logo isiyozidi upana wa 500 na urefu wa 110 (500 x 110px). Logo zote zina weza kuwa zinafanana au kutokana na size unaweza kuweka zikiwa tofauti kidogo. Angalia mfano hapa.

Ili kuweka Logo ingia kwenye sehemu ya Image Manager, kisha sehemu ya kwanza chagua logo yenye zaizi ya (200 x 44px) na sehemu ya pili chagua logo yenye (500 x 110px).

Tovuti Iliyonisaidia Kutengeneza Milioni 20 Mtandaoni

Bofya sehemu ya Browse, kisha bofya Upload kisha baada ya hapa Logo itakuwa imemaliza ku-upload, hakuna haja ya ku-save kwani baada ya kumaliza ku-upload picha itakuwa imemaliza ku-upload moja kwa moja. Sehemu ya mwisho kwenye ukurasa huo huna haja ya kubadilisha chochote.

Sehemu ya DMCA

Kama ambavyo nilikwambia, moja ya kitu ambacho kilifanya niache biashara hii ni kutokana na kupewa request nyingi za DMCA. Kupitia mfumo huu kuna sehemu ya DMCA ambayo itakusaidia kuondoa link ambayo umeambiwa uweze kutoa. Ili kutoa link unatakiwa kubofya sehemu ya DMCA, kisha weka link ambayo unataka kuondoa alafu malizia kwa kubofya Save Settings.

Tovuti Iliyonisaidia Kutengeneza Milioni 20 Mtandaoni

Note : Ni muhimu kuweka link moja kwenye kila mstari yaani weka link moja kisha shuka chini na weka link ya pili na kuendelea, yaani link ziwez zimefuatana.

Jinsi ya Kufanya Website Ifanye Kazi

Sehemu hii ni ya muhimu sana kwani hapa ndipo ubongo wa tovuti hii ulipo, ili kufanya tovuti hii iweze kufanya kazi ni lazima kufanya hatua hii, bila kufanya hatua hii tovuti hii haitoweza kufanya kazi kabisa. Hatua hii ni ya kuweka YouTube API, tovuti hii inatumia baadhi ya api za YouTube ili kuweza kuchukua nyimbo mpya. Unatakiwa kuwa na akaunti ya Google ili kupata API hiyo.

Unachotakiwa kuanya ni KUBOFYA HAPA ukiwa umeingia kwenye akaunti yako ya Google kisha BOFYA HAPA kuangalia jinsi ya kutengeneza YouTube API Data, baada ya kupata YouTube API sasa ingia kwenye tovuti yako na weka API hizo kwenye sehemu hiyo ya Settings, kisha angalia mwisho wa ukurasa huo utaona sehemu iliyo andikwa API Keys.

Paste hapa API Keys zako kisha kama unayo akaunti nyingine ya Google unaweza kutengeneza nyingine na kuziweka hapo pia, unatakiwa uziweka kwa mstari. Kuwa nazo nyingi ni muhimu kwani hizi API huwa zinakuwa na kiwango cha mwisho kwa siku hivyo kama API moja ikifikia kiwango cha mwisho nyingine inaweza kuendelea hadi siku ya kesho yake.

Tovuti Iliyonisaidia Kutengeneza Milioni 20 Mtandaoni

Note : Sehemu hii ni muhimu sana na bila kufanya hivyo tovuti yako haito fanya kazi vizuri, hakikisha unaweka YouTube API kabla ya kuweka tovuti yako mtandaoni. Kama unataka kusaidiwa hili unaweza kuwasilina nasi tutakusaidia kuweka API hizi.

Jinsi ya Kubadilisha Password

Kama ulivyoweza kuona kwenye video hapo juu, password za mfumo huu ni Username Admin na Password ni Admin. Sasa ili kusudi mtu asiweze kuongia kwenye mfumo wako unaweza kufanya mambo haya kubadilisha Password pamoja na kuongeza ulinzi wa tovuti yako. Unaweza kubadilisha password kwa kuingia kwenye file za mfumo wako, hapa sio kwenye admin bali hapo ni pale ambap mafaili ya mfumo huu yanapo patikana.

Tafuta file lililo andikwa includes

Tovuti Iliyonisaidia Kutengeneza Milioni 20 Mtandaoni

Fungua ndani yake utaona file lilo andikwa Config

Tovuti Iliyonisaidia Kutengeneza Milioni 20 Mtandaoni

Baada ya hapo fungua file hilo kisha endelea kwa kuedit sehemu za username na password kama zinavyo onekana kwenye picha hapo chini.

Tovuti Iliyonisaidia Kutengeneza Milioni 20 Mtandaoni

Baada ya hapo save na moja kwa moja utakuwa umebadilisha password pamoja na username ya tovuti yako. Kama umekwama unaweza kuwasiliana nasi kupitia sehemu ya maoni hapo chini na tutakusaidi kuweza kubadilisha hii.

Mambo Mengine Muhimu Sana

Hatua hii pia ni muhimu kwani ngependa ujue kuwa tunaweza kukusaidia kuweka mfumo huu kwenye domain ikiwa pamoja na kusaidia kununua domain yenyewe pamoja na hosting kwa bei nafuu, pia kitu kingine ni kuwa mfumo huu unakuja kwa aina mbili mfumo ambao HAUNA sitemap.xml ambayo ndio inasaidia Google kupata website yako, na mfumo ambao UNAYO sitemap.xml ambayo itakusaidia sana kuanza kutengeneza pesa kwa haraka.

Tovuti ambayo haina sitemap.xml unaweza kupata bure bila kulipia chochote na unaweza kupakua hapo chini. Tovuti ambayo inayo sitemap.xml unaweza kupata kwa kulipia kiasi kidogo cha fedha ambacho kupitia kiasi hicho utaweza kupata mambo yafuatayo.

  • Tutaweza kuinstall mfumo huu kwenye domain yako bure
  • Kama huna domain tutanunua domain unayo itaka bure, utapata pamoja na hosting bila kulipia kiasi cha ziada.
  • Pia tutakusaidia kufanya kila kitu tulicho ongelea kwenye makala hii, ikiwa pamoja na kuweka logo, kubadilisha rangi pamoja na kupata YouTube API.
  • Tutakusaidia kuweka tovuti yako kwenye Google Search.
  • Utaweza kupata akaunti ya matangazo kupitia Propeller Ads pale utakapo kuwa tayari. Pia tutakusaidi kutengeneza mambo mbalimbali yaweze kukaa sawa kwenye tovuti yako.

Kama unataka kupata huduma hii unaweza kuwasiliana nasi kupitia sehemu ya wasiliana nasi mwisho wa tovuti hii. Kwa maoni zaidi hakikisha unauliza kupitia sehemu ya maoni hapo chini na sisi tutajitahidi kujibu maswali yako kwa urahisi zaidi na haraka.

Download Mfumo Huu Hapa

Wasiliana Nasi Hapa

6 comments
  1. kama domain au host ikiisha mda wake inatakiwa kurenew tena? Halafu katika hizo Youtube API mda wake nao ukiisha inakuwaje?

  2. BROTHER NINA OMBA NUMBER YAKO PLEAS MMI NIPO SERIOUS NA HII BIASHARA ULIO ITOA YA KUTENGENEZA PESA KWA BONGO MUSIC PLEAS HELP ME NUMBER YA WATSAPP

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use