Hapa Tanzania Tech tayari tumeshawahi kuongelea njia mbalimbali za kupata pesa mtandaoni ikiwa pamoja na njia za kuanza biashara mtandaoni. Lakini njia zote hizo ambazo tumewahi kuzionyesha kwa namna moja ama nyingine ni lazima itakuta inahusisha tovuti au application ya nje ya nchi hivyo mara nyingi unakuta kama unataka kulipwa ni lazima utalipwa kwa dollar.
Ukweli ni kwamba dollar ni nzuri sana, lakini sio kila mtu mwenye njia ya kuweza kupokea pesa hizo. Tunajua kuwa mara nyingi ili kuweza kupokea hela zako ambazo umetengeneza mtandaoni inakubidi kuwa na akaunti ya benki na tukubaliane na ukweli kuwa, sio watanzania wote wenye uwezo wa kuwa na akaunti za benki na hii ni kutokana na sababu mbalimbali.
Sasa kuliona hili, leo Tanzania Tech tunakuletea njia mpya na rahisi ya kuweza kutengeneza pesa mtandaoni kwa kutumia simu yako ya mkononi. Mbali ya njia hii kuwa rahisi, vilevile pia unaweza kutoa pesa zako kupitia huduma za kifedha za Tigo Pesa, M-Pesa na nyingine. Sasa kabla ujachoka moja kwa moja twende tuangalie njia hii rahisi.
Njia hii inahusisha watumiaji wa simu za Android,na vilevile njia hii inahusisha wewe kupakua application. Kama uko tayari unaweza kubofya link hapo chini itakupeleka kwenye soko la Play Store kisha pakua app hiyo kisha fuata maelezo hapo chini.
App hii ya premise ni app kutoka nje ya nchi ambayo inakupa uweza wa kujibu maswali mbalimbali ambayo utakuwa unalipwa kwa kujibu maswali hayo. App hii inakuja kwa lugha kiswahili pia na inakupa uwezo wa kutuma pesa zako utakazo zipata kupitia huduma za kifedha kupitia simu yako ya mkononi.
Ili kutumia App hii unatakiwa kuwasha GPS kwenye simu yako kwani ni muhimu ili kuweza kujua eneo ambalo unapatikana kwani hii itarahisha kukupatia maswali yanayo lingana na eneo ulilopo. Baada ya hapo unachotakiwa ni kuchagua lugha au app inaweza kugundua yenyewe na kukuletea kishwahili, kisha baada ya hapo sajili akaunti na utaletewa maswali ambayo ndio unatakiwa kujibu ili kupata pesa mtandaoni kupitia simu yako.
Kila swali linakuja na gharama yake hivyo kama swali linahitaji mambo mengi zaidi basi ndivyo hivyo utakavyo lipwa zaidi. Vilevile maswali hayo yana muda maalum hivyo ni muhimu kuyajibu haraka kabla ya muda huo kuisha.
Baada ya kujibu maswali hayo inakubidi kusubiri kati ya siku moja au siku mbili na utawekewa pesa yako kupia app hiyo. Baada ya kuwekewa utaona pesa hiyo kwenye sehemu ya Payment na baada ya kufikisha kiwango kinachotakiwa utakuwa unaweza sasa kutoa kupitia njia mbalimbali za kifedha.
Na hiyo ndio njia mpya ambayo nimekuandalia leo ambayo unaweza kuitumia kutengeneza pesa mtandaoni kwa kutumia simu yako ya Android. Kumbuka njia hii haito kupa mamilioni bali kwa muda utaweza kutengeneza pesa kwaajili ya mambo mbalimbali kwenye maisha yako ya kila siku. Kama kuna mahali umekwama unaweza kutuandikia kupitiasehemu ya maoni hapo chini nasi tutakusaidia.
shukurani sana tanzaniatech.one kwa kutupa faida kama hii.
Karibu sana mahenge.
Tanzania tech,, naombeni mnisaidie jins y kufungua account y PayPal,, nimejaribu nimeshindwa
Unaweza kuuliza swali lako hapa
Naomben mnisaidie jins y kufungua account y PayPal, please
habari..
nimefanikiwa kufungua account ya PayPal nimefanikiwa ila tatizo linakuja kuunganisha kadi yangu ya benki (MasterCard ) kila nikijaribu inashindikana….Msaada tafadhali!!
tunatumiaje app hii ya premise maana sioni kitu nikifungua
yaan inazngua mi kwangu haifanyi kaz
Inawezekana kwa sasa hawana maswali, cha msingi endelea kuwa na hiyo app maswali yatakapo kuju utayapata kwa urahisi zaidi.
duh nyie noma yani kujibu maswali tuu hela mwee mbona watanikoma
inagoma kufunguka mbona
Nini inagoma kufungua
Kwaiyo nikiiingia kwenye play store naandikaje
Sijaelewa swali lako.
Asante sana .nimewasoma vzr
Hii njia ya pay TM ambayo inaunganishwa na simu baada ya hapo nawezaje kutoa hela ili zije mpesa?
Mboni nimefungua lakini imeganda palpale kwenye location tatizo ni nini kwn
samahani nina swali sehemu y kupatiwa pesa yako utaipelekaje kweny mtandao unaoutaka
ndio
je kama mtandao unaotumia wa kupokea pesa hawajauorodhesha unafanyajee ?????
Kivipi uliza swali lako kwa ufasaha zaidi tafadhali.
namaanish wameeka mtandao miwili tuu tigo na vodacom hio mtandao mingine unajiungajee na ukiifikisha kiwango kinachotakiwaah unapelekaje pesa yako kweny mtandao wako ?????
hii app ya premise mbona haikubali ku install?
Ningependa kufahamu Tanzania tech ni muda gani maalum wa kujibu maswali? Na ukipita uo mda wa kujibu maswali je utakuwa umeharibu utaratibu au
Kama unaona swali lako linachelewa kujibiwa unaweza kuuliza swali lako hapa Tanzania Tech forums
Kwa kweli app hii ni nzuri na shukrani Tanzania tech maana mmefungua maisha kwa wale waliopoteza matumaini Katika Marsha.
Maoni*nawezaje kupata app ya payment na nawezaje kuunganishwa na kad yangu ya bank
mbona nimejibu maswali mengi sana lakini sipati pesa
Kivipi, unatakiwa kupata point na hizo point ndio unaweza kuzibadilisha kuwa pesa. Tafadhali fuata maelezo kwenye video.
Maoni* Asante sana tanzania tech, uwepo wenu unatoa nuru kwny maisha ya watu.
Asante na karibu sana.
naitaji kufungua website Lakini nashindwa Naomba usaidizi
Jonasjovin3@gmail.com
0762276275
Maoni*mbona kila siku inataka kurecord eneo lakini haiendelei mbele naomba mnisaidie
Maoni*duu premise app yangu nkifika kwenye location inagoma nafanyej kuongeza accuracy ya location
Naomba kujua nyingine app mbali na Premise.Shukran.
mpo vizuri sana
Maswali Yana ulizwa na Nani? Maybe ananufaikaje?
Sijakuelewa unaweza kurudia swali lako kwa ufasaha zaidi.
Maoni* nashukuru kwa kujiunga nanyie
hi app ya premise mbona inaandika isn’t available to your country? Ni kwang tuu au
Mwezi ulopita nilikuwa naona method ya kutoa pesa kwa mpesa (vodacom) ila sasa hivi imepotea ntapata msaadaa??