Fahamu Mambo Haya Muhimu Kuhusu Password Yako

Fuata sheria hizi kama unataka kutengeneza password ngumu na yenye ubora
Fahamu Mambo Haya Muhimu Kuhusu Password Yako Fahamu Mambo Haya Muhimu Kuhusu Password Yako

Kama wewe ni mtumiaji wa huduma mbalimbali mtandaoni basi lazima unayo password au nywila kwenye huduma hizo unazotumia, mbali ya kuwa kila mtu anamiliki password lakini ni wazi kuwa watu wachache sana ambao wanajua kuwa kuna sheria muhimu ambazo zinaongoza utumiaji wa password ikiwa pamoja na sheria za muhimu za kufuata ili kuwa na password bora na yenye nguvu.

Kupitia makala hii fupi ya leo ningependa nikujuze sheria hizo angalu kwa uchache, sheria ambazo zinaongoza utumiaji bora wa password ikiwa pamoja na utumiaji sahihi wa password au nywila au neno la siri kama inavyo tambulika na watu wengi hapa Tanzania.

Advertisement

Historia ya Password

Kabla ya yote labda turudi nyuma kidogo hadi miaka ya 1960, ambapo ndio inasemekana kuwa password ya kwanza ya kompyuta ilitumika kwenye chuo cha MIT huko nchini marekani. Inasemekana kuwa kipindi hicho kompyuta zilikuwa haziwezi kufanya kazi ya mtu zaidi ya mmoja hivyo ni lazima watumiaji wasubiri mtu mmoja amalize kazi ndipo mtu mwingine aweze kutumia.

Fahamu Mambo Haya Muhimu Kuhusu Password Yako

Swala hilo lilimkasirisha sana mwana sayansi Fernando J. Corbató, ambaye anasemekana kuwa alikuja na mfumo ambao ulikuwa ukiwezesha watumiaji kushirikiana kutumia kompyuta.

Hata hivyo tatizo kubwa la usalama lilizaliwa, Fernando J. Corbató aliamua kutengeneza password ili kutenganisha kazi ya mtumiaji mmoja na mwingine, Huo ndio uliokuwa mwanzo wa Password.

Hata hivyo inasemekana kuwa, Password hiyo ya kwanza ya kompyuta kutengenezwa ndio iliyokuwa password ya kwanza kudukuliwa kwani inasemekana mmoja wa wafanyakazi kwenye maabara ya Fernando J. Corbató, aliona kuwa anahitaji muda wa ziada wa kufanya kazi kwenye kompyuta na hatimaye aliamua kuchapisha password zote zilizokuwa zimehifadhiwa kwenye kompyuta hiyo na kutumia password hizo kuingia kwenye kompyuta hiyo.

Password Ambazo Hupaswi Kutumia

Sasa kwa kuwa tumeongelea “hacked password” hakikisha unakuwa makini sana na password yako na hata siku moja usitumie password inayo fanana na password hizi hapo chini. Hii ni muhimu kwa kuwa password hizo ndio zinaongoza kwa kudukuliwa duniani.

Fahamu Mambo Haya Muhimu Kuhusu Password Yako

  1. 123456
  2. password
  3. 123456789
  4. 12345
  5. 12345678
  6. qwerty
  7. 1234567
  8. 111111
  9. 1234567890
  10. 123123
  11. abc123
  12. 1234
  13. password1
  14. iloveyou
  15. 1q2w3e4r
  16. 000000
  17. qwerty123
  18. zaq12wsx
  19. dragon
  20. sunshine
  21. princess
  22. letmein
  23. 654321
  24. monkey
  25. 27653
  26. 1qaz2wsx
  27. 123321
  28. qwertyuiop
  29. superman
  30. asdfghjkl

Sheria za Password

Sasa mbali ya kuwa password ni neno la siri kwa mtu binafsi na wote tunajua kuwa password ni uamuzi wa mtu, lakini upo muongozo au sheria ambazo zinatumika kuongoza baadhi ya sekta kwenye utumiaji bora wa password. Sheria hizi zipo na zinataka sekta za muhimu kama sekta za serikali na sekta za kiteknolojia kufuata sheria hizo bila kukosea hata kidogo.

Fahamu Mambo Haya Muhimu Kuhusu Password Yako

Kwa mujibu wa Taasisi ya marekani ya Viwango na Teknolojia, National Institute of Standards and Technology (NIST), zipo sheria ambazo ndio zinatumika sasa kwenye nchi mbalimbali ambazo zinatumika kutoa muongozo wa utumiaji bora wa Password. Sheria hizo ni kama zifuatazo.

  • Password inatakiwa kuwa na tarakimu zisizo pungua 8 kama zitatengenezwa na binadamu.
  • Password inatakiwa kuwa na tarakimu zisizo pungua 6 kama zitatengenezwa na kompyuta.
  • Kiwango cha mwisho cha urefu wa password kinatakiwa kuwa tarakimu 64.
  • Alama moja kwenye alama za All ASCII (ambazo ni pamoja na alama za !@#$%^&*()_+) zinatakiwa kuwekwa pale unapo tengeneza password.
  • Password lazima iwe na namba au herufi kubwa moja ama mbili.
  • Unatakiwa kubadilisha Password yako kila baada ya miezi sita.
  • Password haitakiwi kuwa namba zilizo zoeleka, jina la mtu, mahali, barua pepe au kitu.
  • Hairuhisiwi kukosea password zaidi ya mara 10.
  • Hairuhusiwi kutengeneza password ya muda mfupi, yaani password ambayo inaisha muda wake.
  • Hairuhusiwi kumuonyesha mtu maneno ambayo yatamfanya akumbuke password yake (Password Hint).
  • Hairuhusiwi kushare na mtu yoyote password yako.

Hizi ni baadhi tu ya sheria ambazo zime orozeshwa kwenye nakala hiyo, kama unataka kusoma nakala nzima unaweza kusoma hapa.

Jinsi ya Kutengeneza Password Bora

Kama unataka kutengeneza password bora na imara zipo njia mbalimbali unazoweza kutumia, moja ya njia ni kutumia password generetor ambazo pia hutumika kuhifadhi password hizo, unaweza kusoma zaidi hapa kuchagua password generetor bora kwa matumizi yako.

Pia unaweweza kutengeneza password yenye mchanganyiko ya vitu mbalimbali unavyo vijua, kwa mfano unaweza kuunganisha jina la shule uliyosoma ukachanganya na mwaka wako wa kuzaliwa na alama za All ASCII ambazo unaweza kukumbuka kwa urahisi.

Kwa kutumia njia hii utaweza kupata password ngumu yenye ubora ambayo itatumia muda sana kwa mtu au computer kuweza kubashiri au kuhack. Kumbuka kwamba hakuna password ambayo ni salama kwa asilimia 100 hivyo ni muhimu kubadilisha password kila baada ya muda fulani

Kwa ufupi kabisa password ni kitu cha muhimu na kinatunza mambo mengi sana ambayo mengi ya mambo hayo yakiangukia kwenye mikono ya waalifu uleta madhara makubwa. Ni jukumu lako kutengeneza password bora na kuweka ulinzi wa ziada kwenye huduma unazo tumia ili kuhakikisha unakuwa salama hasa mtandaoni. Pia ni muhimu kutunza password yako mwenyewe na usishiriki password na mtu mwingine yeyote.

Kama unataka kujua jinsi ya kuzuia mtu ku-hack akaunti zako za mitandao ya kijamii, basi unaweza kusoma hapa hatua kwa hatua jinsi ya kulinda akaunti zako za instagram, Facebook na Twitter. Kwa habari zaidi kama hizi hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use