Wote tunaijua panasonic kama kampuni ya kutengeneza vifaa mbalimbali vya umeme lakini inawezekana wengi wetu hatujui kuwa kampuni hii pia inajihusisha na utengenezaji wa simu za mkononi maarufu kama smartphone.
Kama ulikua hujui basi ni vyema ukatambua hilo kuanzia sasa kwani hivi karibuni kampuni hiyo imezindua simu zake mbili mpya za bei nafuu huko nchini india. Simu hizo ambazo zina majina ya Eluga Ray 500 na Eluga Ray 700 zimekuja na sifa bora na za kisasa kwa matumizi ya kawaida ya simu janja au smartphone.
Panasonic Eluga Ray 500
Sifa za Panasonic Eluga Ray 500
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 7.0 Nougat
- Ukubwa wa Kioo – 5-inch HD (1280 x 720) IPS | 2.5D curved glass
- Uwezo wa Processor – 1.25 GHz quad-core MediaTek MT6737
- Ukubwa wa Ndani – 32 GB; expandable up to 128 GB with microSD card
- Uwezo wa RAM – 3 GB
- Kamera za Nyuma – Zipo mbili moja inayo Megepixel 8 na 120-degree ultra-wide, nyingine inayo Megapixel 13 huku zote zikiwa na flash ya LED.
- Kamera ya Mbele – Megapixel 5
- Uwezo wa Battery – 4,000 mAh
- Ukubwa wa Simu – 144.26 x 71.26 x 9.2mm
- Uzito wa Simu – 163g
Panasonic Eluga Ray 700
Sifa za Panasonic Eluga Ray 700
- Mfumo wa Uendeshaji – Android 7.0 Nougat
- Ukubwa wa Kioo – 5.5-inch Full HD (1920 x 1080) IPS | 2.5D Corning Gorilla Glass
- Uwezo wa Processor – 1.3GHz octa-core MediaTek MT6753
- Ukubwa wa Ndani – 32 GB; expandable up to 128 GB with microSD card
- Uwezo wa RAM – 3 GB
- Kamera ya Nyuma – 13 MP | Sony IMX 258 sensor | PDAF
- Kamera ya Mbele – 13 MP with flash
- Uwezo wa Battery: 5,000 mAh
- Ukubwa wa simu – 153.75 x 75.35 x 8.9mm
Uzuri wa simu hizi uko kwenye bei simu hizi zinauzwa bei rahisi sana ikiwa na uwezekano wa kununuliwa na karibia kila mwananchi hasa hapa Tanzania.
The Eluga Ray 500 inauzwa kwa dollar za marekani $140 swa na shilingi za kitanzania Tsh 320,000.00 wakati panasonic Eluga Ray 700 ikiwa inauzwa dollar za marekani $155 sawa na shilingi za kitanzania Tsh 350,000. Simu hizi zitaanza kuuzwa rasmi kuanzia kesho tarehe 20 kwenye soko la mtandaoni la Flipkart.
Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa Video.
Chanzo : Android Authority
test