Panasonic Yazindua Televisheni Yenye Kioo Kisichoonekana

Kampuni ya Panasonic imezindua tv yake ya kwanza yenye kioo kisichonekana yani kama Glass
panasonic panasonic

Kampuni maarufu ya Panasonic yenye makao yake makuu huko Osaka nchini Japan hivi karibuni ilizindua TV yake ya kwanza yenye kioo kisichoonekana. Televisheni hiyo ambayo ilikuwa moja kati ya bidhaa mbalimbali zilizokwemo kwenye maonyesho ya CES yanayo fanyika kila mwaka na kampuni hiyo ya panasonic inasemekana ndio Televisheni ya kwanza ya aina hiyo kutengenezwa na kampuni hiyo maarufu ya teknolojia ya Panasonic.

Ikiwa imetengenezwa kwa teknolojia ya HDTV pamoja na OLED televisheni hiyo kutoka Panasonic ina muonekano mzuri ambao pale tu inapo zimwa huonekana kama Glass yenye utupu kabisa yaani (Transparent). Hata hivyo TV hiyo inauwezo wa kuwekwa sehemu yoyote ile kwa mfano TV hiyo inao uwezo wa kufungwa kama kioo cha kabati lako na pale tu TV hiyo inapowashwa hubadilika na kuwa televisheni yenye kuonyesha picha angavu pengine kuliko TV zingine za kawaida.

Advertisement

Kwa sasa kampuni ya Panasonic inafanya bidii kubwa kutengeneza televisheni pamoja na bidhaa mbalimbali zenye kutumia teknolojia za kisasa zaidi ambazo baadhi ya kampuni zilishindwa kutengeneza hapo awali, kwa mfano hapo kampuni ya teknolojia ya Apple nayo ilishwa wahi kutangaza kufanya majaribio ya kutengeneza televisheni zenye kutumia teknolojia hizo za vioo visivyonekana lakini baadae kampuni hiyo ilamua kuachana na majaribio hayo ya kutengeneza televisheni hizo baada ya kuonekana kutumia gharama kubwa za kuwezesha teknolojia hiyo.

Bado haija julikana lini televisheni hizo zitaingia sokoni lakini usiwe na wasiwasi ili kujua bei pamoja na ni lini TV hizo zitaingia sokoni endelea kutembelea blog ya Tanzania tech au unaweza kupata habari zote za teknolojia moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kwa ku-download App ya Tanzania tech  kwenye simu yako ya Android, au pia unaweza kujiunga nasi kwa barua pepe pamoja na mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter, Instagram pamoja na Yotube  ili kupata habari mbalimbali za teknolojia pamoja na kujifunza mambo ya teknolojia kwa njia ya video.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use