Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Jinsi ya Kupata File Lolote kwa Haraka (MP3,MP4,ZIP,PDF,ISO)

Tovuti makini ya kusaidia kupata file la aina yoyote bila matangazo
Jinsi ya Kupata File Lolote kwa Haraka (MP3,MP4,ZIP,PDF,ISO) Jinsi ya Kupata File Lolote kwa Haraka (MP3,MP4,ZIP,PDF,ISO)

Ni wazi kuwa kama wewe ni mwana teknolojia kuna wakati ni lazima utakuwa unahitaji kupata file fulani kwa haraka, iwe una tafuta file za MP3, MP4, ZIP, PDF, ISO au hata file nyingine zozote njia hii inaweza kusaidia sana kuokoa muda.

Kupitia njia hii nimekusogezea tovuti inayokupa fursa ya kupata faili lolote kwa haraka. Tovuti hii ina database kubwa ya faili mbalimbali kutoka kwenye vyanzo mbalimbali. Kwa kutumia tovuti hii, utaweza kupata faili za muziki, video, programu, picha, vitabu au hata file nyingine zozote.

Advertisement

Sasa bila kupoteza muda twende moja kwa moja kwenye njia hii. Sasa ili kupata file lolote kwa haraka kwa kutumia Tovuti hiyo ni rahisi sana. Unachotakiwa kufanya ni kufuata hatua zifuatazo:

1. Ingia kwenye tovuti ya Tovuti hiyo: Kwanza kabisa, ingia kwenye tovuti hiyo kwa kutumia kivinjari chako cha mtandao. Tovuti hii ni bure kabisa na haina gharama yoyote ya usajili, unaweza kubofya hapo chini kutembelea tovuti husika.

Tembelea Tovuti Hapa

2. Tafuta faili unayotaka: Baada ya kuingia kwenye tovuti hiyo, utaona kisanduku cha utafutaji. Hapa ndipo unapoweka jina la faili unayotaka kupata. Unaweza kutumia pia maneno muhimu kama vile jina la msanii au mwandishi.

Jinsi ya Kupata File Lolote kwa Haraka (MP3,MP4,ZIP,PDF,ISO)

3. Chagua aina ya faili: Kwenye kisanduku cha utafutaji, pembeni yake au chini yake utaona chaguo la kuchagua aina ya faili unayotaka kupata (sehemu hiyo imeandikwa All). Unaweza kuchagua kati ya muziki, video, programu, picha na vitabu.

Jinsi ya Kupata File Lolote kwa Haraka (MP3,MP4,ZIP,PDF,ISO)

4. Bofya kitufe cha utafutaji: Baada ya kuweka jina la faili na kuchagua aina ya faili, bofya kitufe cha utafutaji. Na tovuti hii itakupa matokeo ya utafutaji wa faili unayotaka. Kwenye mfano huo mimi nilitafuta file lolote lenye neno “kidato cha nne”.

Jinsi ya Kupata File Lolote kwa Haraka (MP3,MP4,ZIP,PDF,ISO)

5. Pakua faili: Baada ya kupata matokeo ya utafutaji, chagua faili unayotaka kuiweka kwenye kifaa chako. Bofya kitufe cha kupakua na utaanza kupakua faili lako moja kwa moja, kizuri ni kuwa utaweza kuona ukubwa wa file pamoja na mfano wa picha iliyoko ndani kama ni kitabu.

Jinsi ya Kupata File Lolote kwa Haraka (MP3,MP4,ZIP,PDF,ISO)

Kwa kutumia Tovuti hii, utaweza kupata faili lolote kwa haraka na kwa urahisi. Tovuti hii ina database kubwa ya faili mbalimbali kutoka kwenye vyanzo mbalimbali. Unaweza kutumia Tovuti hii kupata faili za muziki, video, programu, picha na hata vitabu. Kwa hiyo, ikiwa unataka kupata faili lolote kwa haraka, basi njia hii ndio njia bora na rahisi zaidi kwako.

Kama unataka kujifunza zaidi unaweza kusoma hapa kujua jinsi ya kuongeza nafasi kwenye kompyuta yako kwa kujua mafile yanayo chukua nafasi kubwa, pia unaweza kusoma hapa jinsi ya kupakua video kutoka mtandao wowote kwa urahisi na haraka.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use