Wote tunajua kuwa uwezo wa teknolojia kwa sasa ni mkubwa sana, vitu tulivyokuwa tunadhani havi wezekani sasa vinawezekana tena vinawezekana zaidi ya tulivyofikiria kudhibitisha hilo labda nikuulize swali, hivi ulisha wahi kuwaza kuwa kidole chako kinaweza kuwa simu ya mkononi.?
Kufanikisha hili nakusogezea hii ya kifaa kipya chenye uwezo wa kubadili kidole chako cha mkono kuwa simu yako ya mkononi, kifaa hicho kinaitwa ORII. ORII ni kifaa ambacho kiko kwenye mfumo wa pete ambapo utakivaa kwenye kidole chako na pale utakapo gusa sikio lako kifaa hicho kita-kuwezesha kupokea simu au kupiga simu moja kwa moja.
Vilevile kifaa hicho cha ORII kinakupa uwezo wa kutuma meseji, kusoma meseji, kuweka kumbukumbu pamoja na vitu vyote ambavyo programu ya SIRI ya Apple pamoja na Google Assitance inavyoweza kufanya.
Kwa kutumia kifaa hicho sasa utaweza kupiga simu bila mtu kusikia unachoongea pamoja na uwezo mkubwa wa kusikia simu yako hata mahali kwenye kelele nyingi. Vilevile kifaa hicho kinakuja na programu za mfumo wa Android pamoja na iOS ambayo utaweza kuchagua ni vitu gani kifaa hicho kifanye.
Kifaa hicho pia kinakuja na uwezo wa battery huku ikiwa na uwezo wa kukaa na chaji kwa muda wa lisaa huku ikichajiwa kwa dakika 45, zaidi ni kuwa kifaa hicho haki-hadhiriwi na maji hivyo ondoa waiwasi pale kinapo pata maji. ORII pia inakuja kwa rangi mbalimbali ambazo zinaendana na kila aina ya nguo. Kwa sasa ORII iko kwenye hatua ya mwisho ili kuanzwa kutengenezwa rasmi tayari kwa kuingia sokoni, unaweza kutoa msaada wako ili kufanikisha kifaa hicho kupitia tovuti ya Kickstarter.
Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.
Chanzo : Android Authority