Kampuni ya Oracle ameripotiwa kushinda mpango wa kusimamia shughuli za TikTok kwa marekani. Oracle ilikuwa sehemu ya mchakato wa zabuni ili kununua TikTok kwa upande wa marekani, lakini tovuti ya The Wall Street Journal inaripoti kuwa kampuni hiyo imechaguliwa kama “mwenzi au msimamizi wa teknolojia anayeaminika na TikTok” badala yake.
Kuwa msimamizi ni tofauti na kununua moja kwa moja mtandao wa TikTok kwa upande wa marekani, na badala yake inaonekana TikTok imependekeza kampuni ya Oracle ndio itasaidia kuendesha shughuli za TikTok kwa marekani kwa kutumia teknolojia za kampuni ya Oracle.
Habari za mpango wa Oracle zinakuja saa moja tu baada ya Microsoft kubainisha kuwa haipo tena kwenye mpango wake wa kununua mtandao wa TikTok kwa marekani baada ya zabuni yake kukataliwa na mmiliki wa mtandao wa TikTok, ByteDance.
Microsoft ilikuwa ikifuatilia mpango wa kununua shughuli za TikTok huko Marekani, Australia, Canada, pamoja na New Zealand.
Hivi karibuni mazungumzo ya wazi yamefanya ununuzi kamili wa TikTok kwa marekani kubadilika kutoka zabuni ya ununuzi kamili, hadi kuwa zabuni ya kuwa mshirika wa teknolojia.
Rais Trump alisaini agizo la utendaji Agosti 6 kuzuia shughuli zote na ByteDance ambayo ndio kampuni mama ya TikTok, na agizo hilo lilitaka kampuni ya marekani kununua biashara ya TikTok kwa upande wa marekani.