Programu maarufu kwa kudhibiti data ya Opera Max iliyokuwa inajulikana na kutumiwa na mamilioni ya watumiaji wa simu za Android ndani na nje ya Afrika hivi leo imebadilishwa na kuanza kuitwa Samsung Max.
Programu hiyo ambayo awali ilikuwa inaitwa Opera Max hapo mwezi wa nane mwaka jana 2017, kampuni ya Opera ambayo pia ni wamili wa kisakuzi cha Opera, walitangaza rasmi kuachana na programu hiyo ya Opera Max ambayo sasa inaonekana kuchukuliwa na kampuni ya Samsung.
Opera Max kwa sasa Samsung Max ni programu inayokupa uwezo wa kudhibiti data kwenye simu yako kwa kuangalia programu zenye kutumia data kwa kiwango kikubwa na kupunguza matumizi yake. Vilevile programu hiyo inasaidia kuweka faragha na kuzuia programu mbalimbali kuweza kuchukua data zako za binafsi ikiwa pamoja na kuzuia programu hizo kumaliza kwa haraka battery ya simu yako.
Kwa sasa wale ambao ni watumiaji wa programu ya Opera Max, watapata toleo jipya la programu hiyo ambayo itabadilka na kuwa Samsung Max. Programu hiyo itakuja na sehemu mpya mbalimbali pamoja na muonekano na sura mpya kabisa. Kama bado huna programu hiyo kwenye simu yako ya Android, unaweza kubofya hapo chini na kupakua programu hiyo kwenye simu yako.