Tangu kuanza kwa mbio za maendeleo ya mifumo ya akili bandia, kampuni ya OpenAI, ambayo ndiyo iliyotengeneza mfumo maarufu wa ChatGPT imekuwamstari wa mbele kuongoza mbio hizo, huku pia ikiwa ni moja ya wafaidika wakubwa na mapato ya teknolojia hii ya Akili bandia.
OpenAI tayari inatajwa kuwa na thamani ya taribani Dola za Kimarekani Bilioni 29 sawa na Takribani Trilioni 72,5 za kitanzania.
Mwaka uliopita, kampuni hiyo iliingiza mapato ya Dola za kimarekani Milioni 28 lakini katika mwaka huu, tayari wanakusanya mapato ya Dola za Kimarekani Milioni 80 kwa mwezi, ili hali matarajio yao kwa mwaka huu yalikuwa Dola za Kimarekani Milioni 200.
Ongezeko hilo la mapato limechangiwa na kuongezeka kwa matumizi ya mfumo wa akili bandia wa ChatGPT, ambao ndio bidhaa nahudumayao kubwa kwa sasa hivi, pamoja na kuuza mifumo mbalimbali ya taarifa kwa makampuni na mashirika ya kiteknolojia ambayo yanaamini maendeleo katika uchakataji wa taarifa kwa mifumo ya akili bandia (Artificial Intelligence) ambayo ndio muelekeo wa sasa katika ulimwengu wa teknolojia.