Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Ongezea Uwezo Programu ya WhatsApp (Chati Ukitembea)

Njia hii ni bora hasa kama uko kwenye maeneo yasio na msongamano
Ongezea Uwezo Programu ya WhatsApp (Chati Ukitembea) Ongezea Uwezo Programu ya WhatsApp (Chati Ukitembea)

Kabla ya kuanza makala hii pengine nikushauri kuwa kuchat huku unatembea sio jambo zuri, lakini kama imekubidi na unatakiwa kujibu meseji za WhatsApp ambazo ni muhimu unaweza kutumia njia hii kuchati huku ukitembela mwendo wa taratibu.

Mbali ya hayo pia kupitia makala hii utaweza kujifunza jinsi ya kuongezea uwezo programu yako ya WhatsApp na kufanya iweze kufanya mambo mengi mbalimbali.

Advertisement

Basi baada ya kusema hayo, moja kwa moja twende nikuonyeshe njia hii rahisi ambayo itakusaidia kuchaji WhatsApp huku ukitembea mwendo wa taratibu na mambo mengine mbalimbali. Kwa kuanza unaweza kuona ni namna gani ambavyo unaweza kuchati huku ukitembea kwa kutumia njia hii.

Kupitia njia hii unaweza kufanya programu ya WhatsApp kuwa transparence na kuweza kutumia kamera ya nyuma ya simu yako kuweza kuona kitu kilichopo chini yako au mbele yako pale unapo tembea.

Ili kupata sehemu hii kwenye programu yako ya kuchati ya WhatsApp, unachotakiwa kufanya ni kudownload app hapo chini. Kisha moja kwa moja fungua app hiyo na fuata maelekezo haya.

MultiBox - Toolkit
Price: Free

Download Hapa

Kwa kuanza fungua programu hiyo kisha moja kwa moja ruhusu permission kwenye programu hiyo kwa kubofya Allow.

Ongezea Uwezo Programu ya WhatsApp (Chati Ukitembea)

Baada ya hapo moja kwa moja bofya kitufe cha Get Started ambacho kipo chini kabisa kwenye programu hiyo.

Ongezea Uwezo Programu ya WhatsApp (Chati Ukitembea)

Baada ua kubofya hapo moja kwa moja utapelekwa kwenye sehemu ya permission ambao unatakiwa kuruhusu programu hii kuonekana juu ya programu nyingine. Utafanya hivyo kwa kubofya kitufe cha switch kilichopo juu upande wa kulia kulingana na simu yako.

Ongezea Uwezo Programu ya WhatsApp (Chati Ukitembea)

Baada ya hapo bofya kitufe cha back kwenye simu yako kisha moja kwa moja utapelekwa kwenye ukurasa wa mwanzo kwenye programu hii. Programu hii inakuja na vitu vingi sana ambayo vinaweza kuongezea uwezo app ya WhatsApp, kama unataka kutembea uku unachat moja kwa moja bofya sehemu iliyo andikwa walk & chat.

Ongezea Uwezo Programu ya WhatsApp (Chati Ukitembea)

Baada ya kubofya hapo utapelekwa kwenye ukurasa wa Accessibility ambapo unatakiwa kuwezesha programu hii moja kwa moja kwenye sehemu hiyo. Moja kwa moja kwenye ukurasa wa Accessibility shuka hadi karibia na mwishoni kisha utaona jina la programu hii na bofya hapo kisha washa kwa kubofya kitufe cha switch na utaona maneno yamebadilika na kuwa ON.

Ongezea Uwezo Programu ya WhatsApp (Chati Ukitembea)

Baada ya hapo moja kwa moja bofya kitufe cha back kwenye simu yako na utarudishwa kwenye programu hii moja kwa moja. Baada ya hapo upelekwa kwenye ukurasa maalum ambao sasa unatakiwa kufungua programu ya WhatsApp kwa kubofya kitufe maalum kwenye app hiyo.

Ongezea Uwezo Programu ya WhatsApp (Chati Ukitembea)

Moja kwa moja bofya hapo na utachagua programu ya WhatsApp kisha baada ya programu ya WhatsApp kufunguaka moja kwa moja utaweza kuona inaonyesha mpaka upande wa pili. Hapo sasa utakuwa ukichati huku ukiwa onaona kilichopo mbele ya simu yako hasa pale unapokuwa unatembea mwendo wa taratibu.

MUHIMU : Ni hatari sana kutembea huku unachati hasa sehemu zenye mkusanyiko wa watu, wanyama, magari au majengo. Ni muhimu sana kuwa muangalifu na hakikisha hauchati huku unatembea kwenye maeneo hayo. Kumbuka njia hii ni kwa ajili ya kujifunza tu na sio vinginevyo. Hatuta husika kwa namna yoyote jinsi njia hii itakavyo tumika.

Kwa kusema hayo basi moja kwa moja natumaini utakuwa umeweza kuchat huku ukitembea taratibu kwenye maeneo yasiyo hatarishi. Kama unataka kujifunza hapa jinsi ya kutumia programu ya WhatsApp kipekee kwa kutumia njia hii rahisi.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use