Karibuni tena kwenye makala nyingine ya Apps nzuri za Android, kama kawaida hapa tunapata nafasi ya kuweza kuangalia Apps nzuri za android ambazo zinaweza kufanya matumizi ya simu yako ya Android kuwa rahisi.
Kama wewe ni mgeni napenda kukukaribisha sana na kama wewe ni msomaji wa makala hizi basi kumbuka unaweza kusoma makala nyingine kama hizi za app nzuri kwa kubofya link inayopatikana mwishoni mwa makala hii.
TABLE OF CONTENTS
Futa Mafaili Yaliyo Jirudia
Kama kwenye simu yako kuna majina yaliyojirudia, picha, nyimbo au hata Video basi app hii itakusaidia kufuta vitu hivyo vilivyo jirudia na kuacha simu yako ikiwa na picha, majina au nyimbo za aina moja yaani ambazo hazija jirudia.
Zuai Vitu Kufutika kwa Bahati Mbaya
App hii ya Dumpster ni app nyingine nzuri sana kwa watumiaji wa simu za Android, App hii inakupa uwezo wa kuzuia kupoteza vitu hasa vile unavyofuta kwa bahati mbaya kwenye simu yako ya Android. Yaani kifupi ni kuwa app hii ni kama vile sehemu ya takataka au Recycle Bin kwenye kompyuta yako, pale unapo futa kitu unaweza kukipata ndani ya App hii.
Ficha Picha na Video kwa Urahisi
Ni kweli kwamba kila mtu anahitaji usiri kidogo kwenye simu yake, iwe huna chochote cha kuficha au hata kama una vitu vya siri ambavyo hutaki watu waweze kuviona ni wazi kwamba usiri ni lazima hasa hasa kwenye sehemu ya picha. App hii ya keepsafe ni muhimu sana kuwa nayo kwani itakupa uwezo pekee wa kuficha picha. App hii haitoficha sehemu ya Gallery bali itaficha baadhi tu ya picha ambazo utakuwa unataka zifichwe na utaweza kuzifungia kwa kutumia fingerprint au hata password.
Fanya SMS au Simu Ijipige kwa Muda Fulani
Hii ni app nzuri sana ambayo itakusaidia kuweza kufanya mambo mbalimbali kwenye simu yako bila kushika simu yako, unaweza kuset app hii iweze kutuma meseji kwa muda flani, pia unaweza kuset app hii ikusaidie kupiga simu kwa muda flani pamoja na kufanya mambo mengine kama kuwasha muziki kwenye simu yako na mambo mengine kama hayo.
Kumbuka Muda wa Kunywa Maji
Maji yana umuhimu sana mwilini, lakini wengi wetu tumekua tukiangalia simu zetu mara nyingi kuliko hata tunavyo kunywa maji. Sasa app Hii itakusaidia kukumbuka kunywa maji ikiwa pamoja na kiasi cha maji unachotakiwa kunywa kwa siku kulingana na uzito wa mwili wako. App hii nzuri sana na itakusaidia kuepukana na magonjwa mbalimbali ambayo husababishwa na ukosefu wa maji.
Fahamu Dalili za Ugonjwa Unaokusumbua
Tukiwa bado tuko kwenye upande huo huo wa Afya, Kama umekua ukijisikia vibaya mara kwa mara na hujui cha kufanya basi App hii ni nzuri sana kwako. App hii itakusaidia kuweza kujua dalili za ugonjwa mbalimbali ushauri mbalimbali wa kiafya pamoja na njia mpya ya kuweza kupata ushauri wa kidaktari bure kupitia simu yako ya mkononi. Kizuri ni kuwa app hii ipo kwa kiswahili.
Fanya Mazoezi Bora Bila Kwenda Gym
Najua kuwa kwenye soko la Play Store kuna app nyingi sana za mazoezi, lakini app hizo nyingi hazija tengenezwa kwaajili ya watanzania wa kipato cha kawaida hiyo ni kutokana na vifaa vinavyo itajika ili kuweza kufanya mazoezi. Hilo ni tofauti kwenye app hii kwani app hii itakupa uwezo wa kufanya mazoezi ambayo hayaitaji wewe uende GYM au kuwa na vifaa vya aina yoyote. App hii itakuonyesha mazoezi ya kawaida lakini yenye nguvu ambayo yatakusaidia kupata mwili mzuri na wenye afya.
Na hizo ndio apps ambazo zinaweza kusaidia sana kuongeza uwezo wa simu yako ikiwa pamoja na kusaidia kwenye maisha yako ya kila siku. Kumbuka apps hizi zote ni muhimu na zinafanya kazi bora sana kwenye simu yako ya Android.
Kama unataka kufahamu apps nyingine nzuri zaidi unaweza kusoma hapa kujua apps nzuri ambazo unaweza kujaribu zaidi kwenye simu yako ya Android.
Kama unataka kujifunza kwa vitendo hakikisha unatembelea channel yetu ya Tanzania tech kupitia kwenye mtandao wa YouTube hapa na utajifunza mambo mbalimbali kwa vitendo. Kwa habari zaidi endelea kutembelea Tanzania tech kila siku.