Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Jinsi ya Kuongeza Speed ya Internet Kwenye Simu Yako

Utaweza kuongeza speed ya Internet kwenye simu yako kwa asilimia kubwa
Jinsi ya Kuongeza Speed ya Internet Kwenye Simu Yako Jinsi ya Kuongeza Speed ya Internet Kwenye Simu Yako

Katika ulimwengu huu wa sasa ni wazi kuwa speed ya internet ni muhimu sana, haijalishi wewe una muda wa kusubiri, au wewe ni kama mimi na ungependa vitu vyote unavyo fungua kwa kutumia smartphone yako vifunguke kwa haraka.

Kama hivi karibuni umekuwa ukifungua app ya Instagram na unaona app hiyo haifunguki au picha zinatumia muda mrefu kufunguka basi upo mahali sahihi. Kupitia makala hii nitakuonyesha njia moja rahisi na ya haraka ambayo itaongeza speed ya Internet kwenye simu yako ikiwa pamoja na kukupa ruhusa ya kutumia baadhi ya tovuti na apps ambazo unaona zimekuwa ngumu kufunguka.

Advertisement

Kumbuka njia hii sio VPN na ni tofauti kabisa na VPN jinsi inavyofanya kazi kwa asilimia 100. Kama unataka kujua jinsi VPN inavyofanya kazi basi unaweza kusoma hapa makala yetu iliyopita.

Kwa kuwa kichwa cha habari kwenye makala hii kinasema “jinsi ya kuongeza speed ya Internet kwenye simu yako”, basi leo sitapoteza muda mwingi kuelezea jinsi njia hii inavyofanya kazi. Kitu cha muhimu ni kufuata maelezo haya mafupi na nakuhahidi utaweza kutumia Twitter na app nyingine bila kuwa na VPN au kitu chochote kama hicho.

Kwa kuanza bofya link hapo chini kisha download app hiyo kwenye simu yako kisha install vizuri kabisa. Kumbuku app hii inapatikana kwenye Android na iOS na unaweza kupata app hiyo kwa kubofya link hapo chini, bila kuja kama unatumia Android au iOS.

Download App Hapa

Baada ya kuinstall na kufungua app hii moja kwa moja, kubali vigezo na masharti ya utumiaji wa app hii, kisha bofya kitufe cha Switch kilichopo katikati, bofya hapo kuwasha app hii.

Jinsi ya Kuongeza Speed ya Internet Kwenye Simu Yako

Baada ya kukubali vigezo vyote ikiwa pamoja na kuwasha sehemu hiyo moja kwa moja utaona alama ya 1 juu ya sehemu ya notification kwenye simu yako. Hiyo ni ishara ya kuwa umemaliza kufanya setup ya app hii na sasa uko tayari kutumia internet kwa speed.

Sasa jaribu kufungua app ya Instagram au app yoyote ambayo ilikuwa slow kama vile Twitter au app nyingine yoyote kwenye simu yako…

Bila shaka umeona kuna mabadiliko, kama kuna tatizo lolote unaweza kutuandikia kupitia sehemu ya maoni hapo chini nasi tutakujulisha njia bora za kutumia app hii. Kumbuka kuwa huwezi kutumia app hii sambamba na VPN hivyo ni lazima kuchagua moja.

Pia kumbuka app hii haifanyi kazi kama VPN bali hii ina angalia zaidi upande wa DNS server na kutokana na kuwa sitaki kukuchosha kwa maneno mengi basi hii itakuwa mada ya siku nyingine.

Kama unataka kujua zaidi mambo mbalimbali ya teknolojia hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania tech kila siku.

7 comments
    1. hii app ya kuongeza speed ya internet kuna wakati app nyingine tofauti na instagram,facebook na twitter zinagoma kufunguka mpaka uifunge ndio app nyengine zinafunguka sasa tatizo ni nini au ndiyo ufanyaji wake wa kazi!

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use