Jinsi ya Kufanya Google Chrome ya Simu Yako Kuwa Haraka Zaidi

google_chrome google_chrome

Kuna wakati unataka kufungua page au website yoyote kwa haraka kwenye simu yako lakini unakuta ndo kwanza browser ya simu yako inakuwa slow sana kiasi kwamba unaweza kukata tamaa au gafla simu yako ika-stack au kuzima na pangine kurestart kabisa, tatizo hili udhaniwa na watu wengi kuwa inawezekana ni virus ambazo ziko kwenye simu au pengine hata kudhani kuwa simu zao ni mbovu hivyo kuzikimbiza kwa fundi moja kwa moja. Lakini kwa kifupi ni kwamba browser za simu zimetengenezwa kwa kiwango maalumu cha kufungua website pamoja na page ambazo ni (Mobile frendly) au rafiki na matumizi ya simu ikiwa ina maana kuwa kuna website au page ambazo hazija tengenezwa maalumu kwaajili ya simu hivyo page hizi hutumia kiasi kikubwa cha memory au (Ram) ambapo hapo hupelekea programu nyingine kushindwa kufanya kazi na kusabisha simu yako ku-stack, kuzima au hata ku-restart.

Lakini je unafanyaje kuzuia tatizo hili..?, Ifuatayo ni njia rahisi ambayo itakufanya uweze kuondokana na tatizo hilo moja kwa moja na kurudisha simu yako kuwa kama hapo awali, kumbuka njia hii ni kwaajili ya wale wanao tumia Google chrome kama (Default) au browser  maalumu ya simu.

Advertisement

Kwa kuanza basi unatakiwa kuhakikisha kuwa Google Chrome kwenye simu yako iko (Update) ukisha fanikisha hilo fungua browser yako ya google chrome kisha fonya kwenye box maalumu la kuandika anuani (URL) kisha andika maneno haya chrome://flags kisha bofya “Go” au “Enter” hakikisha maneno yote unayaandika kwa herufi ndogo, baada ya hapo utaona menu ikiwa na maneno kama kwenye picha hapo chini.

Fanya simu yako kuwa faster

 

Taratibu na umakini tafuta menu yenye maneno haya “Maximum tiles for interest area Mac, Windows, Linux, Chrome OS, Android“  ukisha pata bofya kwenye sehemu iliyoandikwa Default alafu chagua 256 au 512 alfu shuka mpka mwisho wa menu na bofya Relaunch Now. Kwa kufanya hivyo utakua umeondokana natatizo la simu yako kustak au kuzima pale unapotumia Google chrome kama browse ya simu yako na vilevile utaongeza speed ya kufunguka kwa website na page mbalimbali.

Kama mafunzo haya yame kusaidia usisahau kutoa maoni yako hapo chini pia unaweza kuuliza maswali yoyote yanayo husu simu, kompyuta, progamu za simu na mambo mengine yanayo husu teknolojia na tutakujibu hapahapa.

5 comments
  1. Hii ni version gani ya goole chrome kwa sababu kwenye yangu mimi sijaona na nina hili tatizo sana nisaidieni tafadhali..

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use