Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Jiandae na Simu Mpya ya Nokia 5.1 Plus au (Nokia X5) Tarehe 11

Baada ya simu ya Nokia X6 sasa jiandae na simu mpya ya Nokia X5
Tetesi za Nokia 5.1 Plus au Nokia X5 Tetesi za Nokia 5.1 Plus au Nokia X5

Kampuni ya Nokia kupitia HMD Global bado inaendelea na jitihada zake kubwa za kurudi na simu bora na za kisasa. Miezi michache iliyopita kampuni ya Nokia ilizindua simu mpya za Nokia 5.1, Nokia 3.1 na Nokia 2.1, Kama umefanikiwa kusoma makala yetu iliyopita basi lazima utakuwa umeona jinsi simu hizi zilivyokuwa na muonekano mzuri.

Lakini kabla simu hizi hazijafika sokoni vizuri, Hivi karibuni kampuni ya Nokia inategemea kuja na toleo jipya la simu ya Nokia 5.1 Plus au kwa jina lingine Nokia X5, Kwa mujibu wa GSMArena simu hii inakuja ikiwa na muonekano mzuri sana huku ikiwa na kamera mbili kwa nyuma, kioo kikubwa pamoja na ukingo wa juu maarufu kama Notch.

Advertisement

Hata hivyo kwa mujibu wa tovuti hiyo, Nokia 5.1 Plus inakuja na ukubwa wa ndani wa aina mbili kati ya GB 64 pamoja na GB 32, huku processor ya simu hii ikitegemewa kuwa kati ya snapdragon 600-chipset au Helio P60. Nokia X5 au Nokia 5.1 Plus inatarajiwa kuja na uwezo wa RAM za aina tatu kati ya GB 3, GB 4 na GB 6.

Kwenye upande wa Kamera, Simu hii inatarajiwa kuja na kamera mbili kwa nyuma zenye uwezo wa Megapixel 13MP na Megapixel 5MP, kwa upande wa kamera ya Selfie simu hii inakuja na kamera yenye uwezo wa Megapixel 8 huku kwa pembeni ikiwa na sensor mbalimbali.

Hata hivyo simu hii inatarajiwa na kuuzwa kwa Yuan ya China CNY 799 sawa na Tsh 275,000 kwa simu yenye GB 32 huku Yuan CNY 999 sawa na Tsh 345,000 kwa simu yenye ukubwa wa ndani wa GB 64. Kumbuka bei hii inaweza kubadilika kutokana na kodi pamoja na viwango vya kubadilisha fedha vya siku husika.

Kwa sasa simu hii bado haijazinduliwa na inatarajiwa kuzinduliwa rasmi tarehe 11 mwezi huu, huku uwezekano wa simu hii kufika Tanzania ukiwa ni mkubwa kwa sababu siku ya leo kampuni ya HMD Global imeungana na kampuni ya mtandao wa simu ya Tigo Tanzania hivyo ni wazi simu hii na nyingine nyingi labda zinaweza kufika hapa nchini Tanzania kupitia kampuni hiyo.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use