Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Je Wajua Kampuni ya Nokia ilianza Kama Kiwanda cha Karatasi

Historia ya kampuni ya Nokia ni kubwa kidogo kwani ilianza kama kiwanda cha kutengeneza karatasi
nokia nokia

Mwaka 1865 Fredrik Idestam ambaye ndio aliyegundua Nokia alianzisha kiwanda cha kutengeneza karatasi kwenye mji mdogo huko Southern Finland, uanzilishi huu ulifuatiwa na uwazilishi mwingine wa kiwanda kingine kidogo kwenye mji wa karibu wa Nokia hapo mwaka 1868.

Miaka mitatu badae Fredrik Idestam aliamua kubadilisha kiwanda chake kuwa (share company) na ndio hapo kampuni ya Nokia ilipozaliwa rasmi. Hata hivyo kampuni ya Nokia iliendelea kukua ndani ya kipindi chote cha kadre ya 19 hadi hapo mwaka 1960 Nokia ilifungua sehemu ya kampuni yake iliyokuwa ikihusika na electronics. Sehemu hiyo ya kampuni ya Nokia ilikua ikijihusisha na utengenezaji wa vifaa vya kielectoniki iki-wemo redio na simu kwaajili ya jeshi la nchi hiyo.

Advertisement

Mwaka 1979 Nokia ilianza hatua ya kwanza katika upande wa utengenezaji wa simu, hatua hii ilikuja baada ya kampuni hiyo kutengeneza simu yake ya kwanza iliyokua inajulikana kama Mobira Oy, utengenezaji wa simu hii ulifuatiwa na ugunduzi wa simu nyingine ya kwenye gari kutoka Nokia iliyokuwa inaitwa Mobira Senator, simu hii ilifutiwa na simu nyingine iliyokua ikiitwa Mobira Cityman. Simu hii ilikua na uzito wa zaidi ya gram 800 na ilikua ikiuzwa kwa dollar za marekani $6,308 kwa sasa ni sawa na shilingi za Tanzania Tsh 14,000,000.

Miaka ya 90 ndio miaka bora sana kwa kampuni ya Nokia kwani mwaka 1994 kampuni ya Nokia ilitoa simu yake ya kiganjani ya Nokia 2100 iliyokuja na ringtone maarufu ya Nokia inayojulikana mpaka sasa, simu hii ilikuwa ndio chanzo kikubwa cha kampuni hii ya Nokia kuwa maarufu na kupendwa sana. Simu hii iliuza nakala nyingi sana kuliko hata Nokia wenyewe walivyotegemewa hivyo kufanya kampuni hiyo kujulikana na kuwa moja ya kampuni kubwa za utengenezaji wa simu.

Na hiyo ndio historia fupi ya kampuni ya Nokia ambayo ilitoka kutoka utengenezaji wa karatasi mpaka kuwa kampuni kubwa ya utengezaji wa simu za mkonini. Kama una maoni maswali au chcochote kile tuambie kwenye maoni hapo chini au unaweza kujiunga na majadiliano kwenye mitandao yetu ya kijamii ya  Facebook, Twitter na Instagram pamoja na Youtube kama unataka kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video. Pia kama unataka kupata habari zote za teknolojia kwa haraka unaweza kudownload sasa App yetu ya Tanzania tech kutoka Play Store na hivi karibuni itapatikana kupitia App Store.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use