Baada ya kampuni ya Nokia kuingia rasmi kwenye biashara ya TV miezi 6 iliyopita, hatimaye kampuni hiyo hivi leo imetangaza ujio wa TV yake ya pili baada ya TV yake ya kwanza ya Nokia 139.
TV hiyo mpya ya Nokia 43-inch 4K LED Smart TV inakuja ikiwa inatumia mfumo wa Android 9 pie mfumo ambao unawezesha TV hiyo kuwa na uwezo wa kupakua programu kutoka kwenye soko la Play Store.
Mbali na hayo, Nokia 43-inch 4K LED Smart TV inakuja na processor ya CA53 quad-core processor ambayo ina speed ya CPU ya hadi 1.0 GHz. CPU hiyo inasidiwa na RAM ya GB 2.25 pamoja na uhifadhi wa ndani wa hadi GB 16. Kwa upande wa kioo, Nokia 43-inch 4K LED Smart TV inakuja na kioo cha inch 43 kioo ambacho kimetengenezwa kwa teknolojia ya LED huku kikiwa na uwezo wa brightness hadi nits 300 pamoja na uwezo wa teknolojia nyingine kama Dolby Vision, HDR10 na MEMC technology. Pia Nokia 43-inch 4K LED Smart TV inakuja na viewing angle ya hadi digree 178. Kwa upande wa sauti, Nokia 43-inch 4K LED Smart TV inakuja na spika zenye uwezo wa hadi Watt 24W, huku ikiwa na teknolojia ya JBL sound enhancements ambayo inafanya sauti ya TV hiyo kuwa na (sauti nzito) deep bass pamoja na Sauti halisi au (clean vocal tones).
Nokia 43-inch 4K LED Smart TV inakuja na viunganishi vya Bluetooth 5.0, Wi-Fi (yenye 2.4GHz), TV hii inakuja na sehemu tatu za HDMI, na sehemu mbili za USB na sehemu moja ya kuchomeka waya wa internet maarufu kama Ethernet port.
Kwa upande wa bei, Nokia 43-inch 4K LED Smart TV inategemea kupatikana kwanza nchini India na TV hiyo itauzwa kwa Rupee ya India Rs. 31,999 ambayo ni sawa na takribani shilingi za Kitanzania TZS 982,000 bila kodi. Kumbuka bei hii inaweza kubadilika kwa Tanzania.