Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Njia Mpya za Kutumia Mtandao wa Twitter Kwenye Kompyuta

Namna mpya ya kutumia mtandao wa kijamii wa twitter kwa kutumia kompyuta
Njia-mpya-Twitter 2 Njia-mpya-Twitter 2

Kama wewe ni mtumiaji wa mtandao wa Twitter lazima hivi karibuni umeona mabadiliko ya muonekno kwa mtandao huo, mabadiliko hayo yanakuja na njia mpya kabisa za kutumia mtandao huo hasa pale unapokua kwenye kompyuta au hata kwenye simu lakini kwa siku ya leo tutanza kuangalia kwa upande wa kompyuta.

Kwa kuanza ingia kwenye mtandao wako wa twitter kwa kutumia kompyuta yako kisha anza kufuata hatua hizi ili kuweza kupata njia zote za kutumia mtandao huo wa twitter kwa kifupi au kirahisi.

Advertisement

  • Ukitaka kuandika Tweet mpya bofya kibonyezo cha n kwenye kompyuta yako.
  • Kulike Tweet bofya kibonyezo cha I (herufi kubwa) kwenye kompyuta yako.
  • Kujibu Tweet bofya kibonyezo cha r kwenye kompyuta yako.
  • Ku-retweet Tweet bofya kiboyezo cha t kwenye kompyuta yako.
  • Kutuma Direct Message bofya kibonyezo cha m kwenye kompyuta yako.
  • Kuzima Tweet za watu bofya kibonyezo cha u kwenye kompyuta yako.
  • Kublock mtu bofya kibonyezo cha b kwenye kompyuta yako.
  • Kufungua Tweet bofya kibonyezo cha Enter kwenye kompyuta yako.
  • Kufungua picha bofya kibonyezo cha o kwenye kompyuta yako.
  • Kutafuta kitu bofya kibonyezo cha / kwenye kompyuta yako.
  • Kutuma Tweet bofya vibonyezo vya Ctrl kisha Enter kwenye kompyuta yako.
  • Kufungua Menu bofya kibonyezo cha ? kwenye kompyuta yako.
  • Kutembelea Tweet inayofuata bofya kibonyezo cha j kwenye kompyuta yako.
  • Kutembelea Tweet iliyopita bofya kibonyezo cha k kwenye kompyuta yako.
  • Kushuka chini bofya kibonyezo cha space kwenye kompyuta yako.
  • Kufunga Tweet mpya bofya kibonyezo cha – kwenye kompyuta yako.
  • Kurudi kwenye ukurasa wa Home bofya vibonyezo vya g na h kwa pamoja.
  • Kufungua Taarifa au Notification bofya vibonyezo vya g na n kwa pamoja.
  • Kufungua ukurasa wa Mention bofya vibonyezo vya g na r kwa pamoja.
  • Kufungua profile yako bofya vibonyezo vya g na p kwa pamoja.
  • Kuangalia likes bofya vibonyezo vya g na I kwa pamoja.
  • Kufungua ukurasa wa List bofya vibonyezo vya g na i kwa pamoja.
  • Kufungua ukurasa wa messeji bofya vibonyezo vya g na m kwa pamoja.
  • Kufungua ukurasa wa settings bofya vibonyezo vya g na s kwa pamoja.
  • Kufungua ukurasa wa mtumiaji bofya vibonyezo vya g na u kwa pamoja.

Na hizo ndio njia mpya ambazo unaweza kutumia mtandao wa kijamii wa Twitter kwa haraka na kwa urahisi zaidi, kama utakuwa utakuwa umekwama usiache kutuandikia hapo chini nasi tutakujibu moja kwa moja hapa hapa.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use