Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Fahamu nini Maana ya NFC na Jinsi ya Kutumia Kwenye Simu

Hii ndio maana ya sehemu ya NFC inayopatikana kwenye simu yako
Fahamu nini Maana ya NFC na Jinsi ya Kutumia Kwenye Simu Fahamu nini Maana ya NFC na Jinsi ya Kutumia Kwenye Simu

Ni kweli kwamba smartphone nyingi zinakuja na teknolojia mpya na bora nyingine hata ambao hatujui jinsi ya kuitumia. Kama wewe ni msomaji wa tovuti ya Tanzania Tech basi najua utakuwa umesha soma makala kuhusu teknolojia ya Data Roaming ikiwa pamoja na jinsi ya kutumia teknolojia hiyo kwenye simu.

Sasa siku ya leo nimeona tuzungumzie kitu ambacho wengi wetu tumekuwa tukiona kwenye settings za simu zetu lakini tumekuwa tukishindwa kujua nini maana ya kitu hicho ikiwa pamoja na jinsi ya kutumia. Kitu hicho sio kingine ni sehemu ya NFC.

Advertisement

Kwa wale wenye simu za kisasa hasa Android, bila shaka sehemu hii imekuwa ni sehemu ya kawaida kuiona kwani mara nyingi imekuwa ikipatikana juu kabisa kwenye uwanja wa taarifa au (Notification Panel). Kama inavyoweza kuonekana kwenye picha hapo chini.

Fahamu nini Maana ya NFC na Jinsi ya Kutumia Kwenye Simu

Mara nyingi sehemu hii huwa imeandikwa NFC uku ikiwa imechrowa alama ya N ikiwa na ishara kuwa simu hiyo inayo teknolojia hiyo. Sasa sio kila simu inakuja na teknolojia hii hivyo ni vyema kuangalia alama hiyo kwenye settings za simu yako kujua kama simu yako inakuja na teknolojia hiyo.

Nini Maana ya NFC ?

Kwa kirefu NFC maana yake ni Near-field communication, kwa lugha ya Kiswahili hii ni Mawasiliano ya Karibu au yanayokaribiana. NFC ni mfumo wa mawasiliano ya karibu ambao huwezesha vifaa viwili vya kielektroniki, kama vile smartphone, kuanzisha mawasiliano kwa kuwa karibu takribani sentimita 4 ya kila kifaa.

NFC Inapatikana Wapi

Mara nyingi teknolojia ya NFC inapatikana kwenye vifaa vya kieletroniki kama vile simu za mkononi ambazo ni simu janja au (Smartphone), pia unaweza kukuta teknolojia hii kwenye vifaa vya malipo ya kielektroniki kwa mfano EFD, Mashine za kupokea malipo kwenye maduka kama SuperMarket na sehemu nyingine kama hizo.

Je NFC Inatumikaje

Kama nilivyo kwambia hapo juu, NFC hutengeneza mawasiliano kati ya vifaa viwili ambavyo vimekaribiana, hii ni sawa na kusema teknolojia hii inauwezo wa kufanya kila kitu ambacho Bluetooth inafanya ikiwa na mambo mengine ya ziada kama vile kufanya malipo kwa haraka pamoja na mambo mengine makubwa zaidi.

Je Kuna Tofauti Gani Kati ya Bluetooth na NFC

Bluetooth na NFC hii yote ni mifumo inayotumika kufanya mawasiliano baina ya vifaa viwili kwa ukaribu, lakini NFC yenyewe ufanya kazi kwa umbali usiozindu Sentimita 4, wakati Bluetooth yenyewe hufanya kazi kwa umbali takribani sentimita 13 au zaidi. Unaweza kuona kama teknolojia ya Bluetooth ni bora kuliko NFC, lakini tukija upande wa teknolojia NFC imetengenezwa kisasa zaidi kuliko Bluetooth.

Faida nyingine ya NFC ni kuwa, teknolojia hii haitaji kuunganishwa na mtu, ila unachotakiwa kufanya ni kuwasha tu sehemu hiyo ya NFC kwenye vifaa vyote viwili na moja kwa utaweza kuunganisha vifaa viwili. Bluetooth kwa upande mwingine yenyewe ni lazima kuunganisha kwa kubofya sehemu maalum ili kuruhusu kuunganisha vifaa viwili.

Tofauti na hayo, tofauti iliyopo kati ya Bluetooth na NFC ni katika swala zima la teknolojia, ila vyote hufanya kazi kwa pamoja, kwa mfano simu nyingi za .

Je Unawezaje Kutumia NFC kwenye Simu Yako

NFC mara nyingi hutumika kwenye simu kufanya mambo mbalimbali, Kwenye simu za siku hizi kwa mfano Samsung, NFC hutumika kuwezesha kufanya malipo kwa haraka kwa kuweka simu yako mahali kwenye teknolojia hiyo na pia NFC hutumika kufanikisha baadhi ya teknolojia kama vile teknolojia za kufungua milango kwa kutumia simu pamoja na mambo mengine mengi.

Sasa kama simu yako inayo sehemu ya NFC, unachotakiwa kufanya ni kuwasha sehemu hiyo kisha washa sehemu hiyo pia kwenye simu nyingine baada ya hapo fanya kama unataka kutuma kitu kwa kutumia Bluetooth na moja kwa moja gusanisha simu zote mbili na moja kwa moja utaona kitu hicho kinatumwa kwenda simu nyingine.

Hayo ndio maelezo mafupi kuhusu NFC, Natumaini hadi hapo utakuwa umepata idea ya nini maana ya NFC, ikiwa pamoja na njia rahisi ya kutumia teknolojia hiyo. Kama kwa namna yoyote itakuwa kuna mahali hujaelewa usiache kuuliza swali lako kupitia maoni hapo chini.

2 comments
  1. Mi nakushukuru sana,sana.ni mda mfupi sana nimeanza kufuatilia post zako.ila nimefanikiwa kujua mambo mengi ya kwenye Simu ambayo mwanzo nilifikiri kuwa yako mbali sana.hitaji language kubwa kwa sasa Nina wazo LA kuanzisha huduma ya ufundi Simu kwenye category ya Ku flash,unlock may be kubadilisha imei,kutoa password, pin,Frp..na mengine yafananayo na hayo.je,napaswa kuanzia wapi,au wewe mwenyewe uko tayari kunifundisha?asante.Niko dar

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use