WhatsApp ni programu muhimu sana kuwa nayo siku hizi, lakini kama zilivyo programu nyingine programu ya WhatsApp nayo sio perfect kwa asilimia 100 kwani kuna mambo mengi sana ambayo pengine watu wanahitaji lakini wanayakosa kupitia programu ya WhatsApp ndio maana watu hugeukia programu kama za GBWhatsApp na WhatsApp Plus.
Kwa wale ambao hamjui kuhusu programu ya GBWhatsApp na WhatsApp Plus hizi ni programu za WhatsApp ambazo sio rasmi, programu hizi zimetengenezwa kama programu rasmi ya WhatsApp na zinakupa uwezo zaidi kwa kuongezewa baadhi ya vitu kwenye programu rasmi ya WhatsApp vitu ambavyo havipo kwenye programu ya hiyo rasmi ya WhatsApp.
Programu hizo zinaongeza vitu mbalimbali kama vile uwezo wa kuzuia mtu kublock akaunti yako, uwezo wa kubadilisha kabisa muonekano wa programu ya WhatsApp, unaweza kuwasha sehemu ambayo itakuonyesha uko hewani kwa muda wa masaa 24, vilevile utaweza kutuma video zenye ukubwa wa zaidi ya MB 50 pamoja na mambo mengine mengi.
Lakini pamoja na kuwa na mambo mengi mazuri yapo maswali mengi sana mtandao yanayo hoji kama utumiaji wa programu hizi za GBWhatsApp pamoja na WhatsApp Plus kama ni salama, maswali hayo mengi yanaelekezwa kwa programu ya GBWhatsApp kwani kwa sasa ndio programu inayotumiwa na watu wengi ukilinganisha na WhatsApp Plus. Lakini kabla ya kukwambia kama programu hizi ni salama ama lah! labda nikwambie jinsi programu hizi zinavyofanya kazi.
Kwa kuanza labda nikwambie kuwa programu za aina hii mara nyingi zinaitwa Mods Apps au kwa lugha ya kompyuta maana yake ni modification na kwa kiswahili ni tafsiri yake ni Mabadiliko. Sasa mara nyingi programu za aina hii hutengenezwa juu ya programu rasmi na kuongezewa baadhi ya vitu kwa kubadilisha baadhi ya code ndani ya programu rasmi ili kuweza kukupa sehemu za ziada kama zile zinazopatikana kwenye programu za GBWhatsApp na WhatsApp Plus.
Sasa kwa upande wa GBWhatsApp programu hii mpaka sasa inatumiwa na watu wengi sana na bado hakuna taarifa za mtu kufungiwa akaunti kwaajili ya kutumia programu hiyo. Lakini kwa upande wa WhatsApp Plus mambo ni tofauti kidogo, Mwaka 2015 WhatsApp iliwafungia kwa masaa 24 watumiaji wote wa programu ya WhatsApp Plus, sababu kubwa ilikuwa ni kukiuka vigezo na masharti pamoja na matumizi mabaya ya programu ya WhatsApp kwa ujumla.
Sasa moja ya vigezo na masharti yaliyovunjwa na waandishi wa programu ya WhatsApp Plus ni pamoja na watengenezaji wa programu hiyo kufanya mabadiliko ya code za muhimu za programu rasmi ya WhatsApp ili kuweza kuongeza baadhi ya mambo kwenye programu hiyo ya WhatsApp Plus. Mabadiliko hayo yalikuwa yanahusisha code maalum za WhatsApp zinazoitwa Core Code.
Core Code hizi ni code zinazolidwa sana na WhatsApp na hizi ndio zinabeba mambo muhimu yanayopatikana kwenye programu rasmi ya WhatsApp. Mabadiliko yoyote yanayofanywa kwenye core code huo ni mabadiliko yanayo adhiri programu ya WhatsApp kiusalama pamoja na kiutumiaji, hivyo mabadiliko yoyote yanayofanywa na watu ambao sio watengenezaji rasmi wa programu ya WhatsApp ni kosa kisheria na pia ni hatari kwa watumiaji wa programu hiyo kiusalama.
Kwa upande wa GBWhatsApp, watengenezaji wake wako makini na hawajawahi kubadilisha sehemu hii ya Core Code bali wao hubadilisha code ambazo zinatumika kuonyesha muundo wa programu hiyo rasmi ya WhatsApp pamoja na sehemu nyingine za kawaida ambazo mara nyingi hizi huwa hazilindwi kwenye programu yoyote ya Android.
Kwa kuona hivyo utajua kuwa, programu ya WhatsApp inakuwa sio salama endapo Core code za programu hiyo zikibadilishwa kwa namna yoyote hivyo hadi hapo unaweza kuona kuwa pengine hii ndio sababu hadi sasa watu wanaendelea kutumia programu ya GBWhatsApp. Sasa tukija kwenye majibu ya maswali kama programu hizi ni salama..
- Je GBWhatsApp na WhatsApp Plus ni Salama ?
Kwa mtu yoyote ambaye yuko makini na usalama wake hasa mtandaoni ni muhimu sana kuhakikisha unajilinda bila kujali kwa sasa wewe ni mtu wa aina gani. Nimesema bila kujali wewe ni mtu wa aina gani kwa sababu kuna dhana kwamba mtu anasema yeye sio mtu muhimu wala hafanyi biashara yoyote mtandao hivyo hana sababu ya kujilinda mtandao, dhana hii ni potofu kwani huwezi kujua utakuwa wapi kesho hivyo ni vizuri kuweka usiri kwenye maisha yako ya sasa usije ukaadhiri maisha yako ya baada au maisha ya watoto wako.
Programu za GBWhatsApp na WhatsApp Plus hazina uhakika kwa asilimia 100 kama ni programu salama, hivyo kwa ushauri wangu kama unatumia programu hizi kwa mambo yako ya siri ni vyema kuacha kutumia programu hizi mara moja. Programu hizi pia zinaweza kutumika kufanya mambo mbalimbali kwenye simu yako kama vile kuweka uwezo wa kuwasha mic ya simu yako hivyo kusikiliza unachokisema kila mara pamoja na kuchukua data za matumizi ambazo kwa kawaida haziruhusiwi kuchukuliwa na programu mbalimbali za simu.
Mbali ya hayo kwa kutumia programu za GBWhatsApp na WhatsApp Plus unaweza kufungiwa kutumia namba hiyo kwenye WhatsApp ya kawaida na kufanya ushindwe kufanya mambo yako ya msingi kwa kutumia programu ya WhatsApp ambayo ni inategemewa sana siku hizi. Hakuna sababu ya kuwa na mashaka pale unapotumia programu kwa kuofia data zako kuchukuliwa hivyo ni muhimu kuwa makini na programu unazopakuwa kwenye simu yako.
Japo kuwa watumiaji wa programu ya GBWhatsApp hawajawahi kufungiwa kwa kutumia programu rasmi ya WhatsApp, ila bado ziko hatari nyingi sana za kutumia programu hizo kwani huwezi kujua ni data gani ambazo wabunifu wa programu hiyo wanachukua. Japokuwa WhatsApp rasminayo inaweza kuwa inafanya hivyo ila pengine ni tofauti kwani ni rahisi kuwajibisha kampuni kuliko kuwajibisha mtu mmoja au watu ambao huwajui. Kumbuka ni imeandikwa kwenye vigezo na mashari kuwa husutumie programu hizo ambazo sio rasmi hivyo pale utakapo pata tatizo WhatsApp haita husika kwa namna yoyote kukulipa au kutatua tatizo lako.
Natumaini hadi hapo utakuwa unajua kama programu hizi ni salama au lah..! kama wewe ni mtumiaji wa programu ya GBWhatsApp na WhatsApp Plus labda utuambie hapo chini kwenye maoni ni sababu gani inayokufanya kuhamia kwenye programu hizo na ni sehemu gani unayo ipendelea zaidi kwenye programu hizo.
je vipi kuhusu Yowhatsapp na Fm whatsapp ambazo pia zinaenda features na zile za Gbwhatsapp?
Jacob makala hii ni kwaajili programu zote tu za WhatsApp kama hizo.
Ahsante kwa makala
Habari admin, mi natumia parallel space kwa ajili ya WhatsApp nyingine yaani natumia simu moja kwa WhatsApp mbili je hii ina madhara gani kwenye simu!?
Maoni*jee kama sisi ni waathilika wa whatsap gb na namba imeshakuwa bunn tunatakiwa tufanyaje ili namba zetu zifanye kazi tena
Thanks for awareness of GB what’s app.
Ikiwa GB what’s app ipo na vitisho vya aina hii basi waaanzilishi wa What’s app na wao wawe update kutuwekea muundo wa kisasa kama ilivo GB what’s app ili kuokoa taifa kuenda ktk majanga