Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Sasa Unaweza Kutumia Ngozi ya Mwili Kama Touch Screen

Unaweza Kutumia Ngozi Yako Kama Touch Screen kwa Simu Yako
touch screen touch screen

Smartwatch au saa janja za mkononi mara nyingi huonekana ni bora kutokana na uwezo wa kuendesha saa hiyo ina pokua mkononi, lakini wataalamu katika chuo cha Carnegie Mellon uko Pennsylvania marekani wamegundua teknolojia mpya aliyopewa jina la “SkinTrack” ambayo unaweza kuendesha saa hiyo kwa kutumia ngozi ya mwili wako.

Advertisement

Hata hivyo sehemu ya kikundi kilicho tengeneza teknolojia hiyo cha Future Interfaces Group, kilisema saa hiyo imetengenezwa na m-kanda maalum ambao ndio unatoa mawasiliano au “high frequency AC signal” kutoka kwenye mkono kwenda kwenye saa hiyo. Wakieleza jinsi saa hiyo inavyofanya kazi wataalam hao waliendelea kusema kuwa unaweza kutumia saa hiyo kwa kuweka saini kwenye ngozi au kufungua baadhi ya programu flani kwenye simu yako kwa kuji chora na kidole kwenye sehemu ya ngozi ya mkono uliyovaa saa hiyo, pia unaweza ukatoa programu yako kwenye simu na kwenda kwenye saa hiyo kwa kuchika kwenye simu na kwenye sehemu ya ngozi ya mkono uliyo vaa saa hiyo.

Hata hivyo teknolojia hiyo bado haija wekwa kwa ajili ya kuingia sokoni bali chuo hicho kimesema siku za karibuni teknolojia hiyo itatumiwa kutengeneza saa janja kwaajili ya simu za mkononi.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use