MIT Yaja na Nepi ya Kidigitali Inayotoa Taarifa Ikiwa Imechafuka

Mbali ya yote sensor hiyo haitumii batter wala chanzo chochote cha umeme.
MIT Yaja na Nepi ya Kidigitali Inayotoa Taarifa Ikiwa Imechafuka MIT Yaja na Nepi ya Kidigitali Inayotoa Taarifa Ikiwa Imechafuka

Watafiti kutoka chuo cha MIT hivi karibuni wamegundua sensor ndogo inayoitwa RFID ambayo inao uwezo wa kugundua unyevu unyevu kwenye nepi ya mtoto. Sensor hiyo ndogo inao uwezo wa kutuma mawimbi ya mawasiliano (signal) kwenye kipokezi au receive iliyopo karibu na hivyo inaweza kumpa taarifa mzazi pale nepi ya mtoto inapokuwa chafu.

Kwa mujibu wa tovuti ya MIT, inasemekana kuwa sensor hiyo inaweza kutengenezwa kwa gharama ndogo sana ambazo zinafikia chini ya sent 2 za marekani ikiwa ni sawa na takribani TZS 463, hii inafanya uwezekano wa nepi hizo kutumika mara moja na kutupa zikiwa na sensor hiyo ndani yake, hiyo pia inafanya gharama za nepi hizo kuwa chini zaidi.

Advertisement

MIT Yaja na Nepi ya Kidigitali Inayotoa Taarifa Ikiwa Imechafuka

Kwa mujibu wa MIT, sensor hiyo mpya huchanganywa na hydrogel typically ambayo hutumiaka kutengeneza nepi za watoto na pale nepi hiyo inapo jaa na kupata unyevu unyevu sensor hiyo hupanuka na kutuma mawimbi ambayo upokelewa na kipokezi ambacho hutuma taarifa kwa mtu aliye karibu. Mbali ya yote sensor hiyo haitumii batter wala chanzo chochote cha umeme.

Kwa sasa, Sensor huyo bado inafanyiwa majaribio ya awali na pengine kwenye miaka ya karibuni utaweza kuletewa taarifa kwenye simu yako ya mkononi pale unapo takiwa kubadilisha nepi ya mtoto wako. Kama unataka kujua zaidi, soma hapa kufahamu mambo mengine sita ya teknolojia ambayo huwenda ulikuwa hujui.

Kwa habari zaidi endelea kama hizi endelea kutembelea Tanzania Tech kila siku pia usisahau kujiunga nasi kwenye kwa ku-subscribe kwenye channel yetu kupitia mtandao wa YouTube Hapa.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use