Nearby Share : Njia Mpya ya Kutuma na kupokea Mafile

Fahamu sehemu mpya ya kutuma na kupokea mafile kwa urahisi na haraka
Nearby Share : Njia Mpya ya Kutuma na kupokea Mafile Nearby Share : Njia Mpya ya Kutuma na kupokea Mafile

Baada ya miaka kadhaa hatimaye kampuni ya Google imeleta njia mpya ya kutuma na kupokea mafile kwa haraka kama ilivyo AirDrop ya mfumo wa iOS. Sehemu hiyo mpya ambayo inaitwa Nearby Share.

Sehemu hii inategemewa kuwezeshwa kwenye simu zote za Android zenye mfumo kuanzia Android 6 (Marshmallow) na kuendelea.

Advertisement

Kupitia sehemu hiyo mpya ya Nearby Share utaweza kutumia file lolote kwa haraka kupitia simu iliyo wezeshwa. Utaweza kutuma mafile kwa haraka kama simu yako imeunganishwa na WiFi au Bluetooth na location au vyote kwa pamoja.

Jinsi ya Kuwezesha Nearby Share

Hadi sasa tayari Google imesha tangaza rasmi ujio wa sehemu hii kwenye simu zote zenye Android 6 na kuendelea bila kujali aina ya kifaa. Kama wewe ni mmoja wa watu wanaotumia simu au kifaa chochote chenye mfumo wa Android kuanzia Android 6 (Marshmallow) na kuendelea basi tegemea kupata sehemu hii kwenye kifaa chako moja kwa moja.

Kuhusu njia ya kuwezesha sehemu hii, huna haja ya kufanya chochote kitu cha muhimu subiri na sehemu hii itawezeshwa na Google bila wewe kufanya kitu chochote. Kumbuka, ili kutumia sehemu hii unahitaji kuwasha WiFi, Bluetooth pamoja na Lacation kwenye kifaa chako.

Jinsi ya Kupata Sehemu ya Nearby Share

Najua kuwa unajiuliza baada ya sehemu hii kuwezeshwa kwenye simu yako je utajuaje kama sehemu hii inapatikana kwenye kifaa chako.? Kujibu swali hili unaweza kufanya yafuatayo kuweza kuona kama sehemu hii imewezeshwa kwenye simu yako.

  • Kupitia sehemu ya Notification Panel iliyopo juu kabisa kwenye simu yako, vuta hapo kisha nenda mpaka kwenye sehemu ya Notification Icons kisha bofya sehemu ya EDIT. Sasa sehemu hii nitofauti kwa kila simu hivyo ni muhimu kujua mahali ambapo utaweza kuedit icon kwenye simu yako.
  • Njia ya pili ni kupitia sehemu ya kushare, unatakiwa kufanya kama unataka kushare kitu na moja kwa moja utaweza kuona sehemu ya Nearby Share ikiwa kama moja ya sehemu ya kushare file au kitu chochote.

Nearby Share : Njia Mpya ya Kutuma na kupokea Mafile

  • Njia nyingine ya mwisho ya kujua kama sehemu ya Nearby Share imewezeshwa kwenye simu yako unaweza kuangalia kupitia sehemu ya Google kwenye settings ya simu yako. Unachotakiwa kufanya ni kuingia kwenye sehemu ya Settings > Google > Tafuta Device Connections > kisha utaona Nearby Share kwenye list.

Kama ukiona sehemu hii basi sehemu hii itakuwa imewezeshwa kwenye simu yako na unaweza kuendelea kuitumia kwa urahisi kwenye kifaa chako cha Android 6 na kuendelea.

Jinsi ya Kuedit Profile Yako ya Nearby Share

Nearby Share hutuma mafile pamoja na profile yako kwa mtu yoyote unae share nae mafile au data yoyote. Hii ikiwa pamoja na jina la profile yako pamoja na picha. Mara nyingi sehemu hii huchukua picha yako kutoka kwenye akaunti yako ya Google, pamoja na jina la kwanza la akaunti yako ya Google. Lakini pamoja na hayo unaweza kuedit profile yako kwa urahisi.

Kama unataka kuedit unaweza kufuta njia hizi rahisi, ingai kwenye sehemu ya Settings > Google > Tafuta Device Connections > kisha utaona Nearby Share kwenye list. Bofya hapo na moja kwa moja utaweza kuanza kuedit jina pamoja na profile yako kwa urahisi.

Kwa kugusa sehemu iliyo andikwa Device name utaweza kubadilisha jina ambalo litakuwa linaonekana pale mtu atakapo kuwa anapokea data kutoka kwako. Kwa kugusa sehemu ya picha utaweza kuongeza au kubadilisha akaunti yako ya Google ambayo ndio inakuja na picha ambayo inatokea pale mtu atakapokuwa anapokea data kutoka kwenye simu yako.

Pia utaweza kuadilsha upatikanaji wa sehemu hii kwa kubadilisha sehemu iliyo andikwa Device visibilty. Pia unaweza kubadilisha vitu zaidi pale unapokuwa umewasha sehemu hiyo. Unaweza kuwasha kwa kubofya sehemu ya Turn on iliyopo chini kulia kama inavyo onekana kwenye picha hapo chini.

Nearby Share : Njia Mpya ya Kutuma na kupokea Mafile

 

Hadi hapo natumaini utakuwa umefahamu vizuri sehemu ya Nearby Share, kama simu yako inayo Android 6 na bado haina sehemu hii usijali kwani sehemu hii inakuja kwa awamu na utaweza kupata sehemu hii ndani ya siku za karibuni.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use