Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Je Wajua Korea Kusini Ndio Nchi Yenye Internet Yenye Kasi Zaidi

Hivi karibuni inatarajia kuongeza kasi hadi GB 2.5 kwa sekunde
Korea Kusini Nchi Kasi ya Internet Korea Kusini Nchi Kasi ya Internet

Moja kati ya kitu kinacho changia maendeleo kuja kwa haraka kwa sasa ni uwezo wa internet kwenye eneo husika, ukiangalia nchi nyingi zilizo endelea nyingi zinauwezo mzuri wa internet na mawasiliano kwa ujumla. Lakini pamoja na hayo ni wazi kuwa nchi yenye kasi kubwa ya internet ni lazima pia itakuwa na uwezo mkubwa wa kiteknolojia pamoja na uwezo mkubwa wa kimawasiliano.

Kuliona hilo leo nimekuletea list hii ya nchi zenye kasi kubwa ya internet dunia pamoja na nchi zenye kasi ndogo ya internet duniani, bila kusahau nchi za Afrika zenye kasi kubwa ya internet. List hii imetokea kwenye vyanzo mbalimbali vya kuaminika ikiwa pamoja na (Akamai Q1 2017 global average connection speeds rankings), (IT News Africa) pamoja na (The Atlas).

Advertisement

  • Nchi Zenye kasi Kubwa ya Internet Duniani

5. Norway – Nchi ya Norway hadi kufikia mwezi may mwaka jana 2017 ilikuwa na uwezo wa internet yenye kasi ya MB 21.7 kwa sekunde.

4. Hong Kong – Nchi ya Hong Kong hadi kufikia mwaka jana 2017 ilikuwa na uwezo wa internet yenye kasiya MB 21.9 kwa sekunde.

3. Sweden – Nchi ya Sweden hadi kufikia mwaka jana 2017 ilikuwa na uwezo wa internet yenye kasi ya MB 22.5 kwa sekunde.

2. Switzerland – Nchi ya Switzerland hadi kufikia mwaka jana 2017 ilikuwa na uwezo wa internet yenye kasi ya MB 23.5 kwa sekunde.

1. South Korea – Nchi ya South Korea, au Korea ya kusini ndio inashika kinara kwa kuwa na internet yenye kasi ya MB 28.6 kwa sekunde. Mbali na kasi hiyo kwa mujibu wa tovuti ya CNET hivi karibuni korea kusini imetangaza kuzindua Internet yenye kasi ya GB 2.5 kwa sekunde. Ndio umesoma sahihi yaani filamu ya GB 1 ukiwa korea ya kusini unaweza kuipakuwa kwa chini ya sekunde moja..

  • Nchi Zenye Kasi Ndogo ya Internet Duniani

5. Somalia – Nchi ya Somalia hadi kufikia mwezi wa tano mwaka jana 2017 ilikuwa na internet yenye kasi ya MB 0.62 kwa sekunde.

4. Congo – Nchi ya Congo hadi kufikia mwezi wa tano mwaka jana 2017 ilikuwa na internet yenye kasi ya MB 0.55 kwa sekunde.

3. Burkina Faso – Nchi ya Burkina Faso hadi kufikia mwezi wa tano mwaka jana 2017 ilikuwa na internet yenye kasi ya MB 0.49 kwa sekunde.

2. Gabon – Nchi ya Gabon hadi kufikia mwezi wa tano mwaka jana 2017 ilikuwa na internet yenye kasi ya MB 0.41 kwa sekunde.

1. Yemen – Nchi ya yemen ndio yenye kasi ndogo ya internet hadi kufikia mwezi wa tano mwaka jana 2017 nchi hiyo ilikuwa na internet yenye kasi ya MB 0.34 kwa sekunde. Kama unavyo ona nchi nyingi hapo ni za Afrika hivyo sina haja ya kukwambia list ya nchi za Afrika zenye kasi ndogo ya internet.

  • Nchi za Afrika Zenye Kasi Kubwa ya Internet

Kwa upande wa Afrika hapa napenda nikujuze kuwa ifuatayo ni list ya nchi kumi zenye uwezo mkubwa wa internet kwenye upande mzima wa kudownload.

10. Uganda – Uganda inashika namba kumi kwa kuwa na kasi ya internet ya kudownload MB 2.12 kwa sekunde.

9.  Ghana – Ghana inashika namba tisa kwa kuwa na kasi ya internet ya kudownload ya MB 2.3 kwa sekunde.

8. Zambia – Zambia inashika namba nane kwa kuwa na kasi ya internet ya kudownload ya MB 2.45 kwa sekunde.

7. Zimbabwe – Zambia inashika namba saba kwa kuwa na kasi ya internet ya kudownload ya MB 2.49 kwa sekunde.

6. Nigeria – Nigeria inashika namba sita kwa kuwa na kasi ya internet ya kudownload ya MB 3.15 kwa sekunde.

5. Madagascar – Madagascar inashika namba tano kwa kuwa na kasi ya internet ya kudownload ya MB 3.49 kwa sekunde.

4. Tunisia – Tunisia inashika namba nne kwa kuwa na kasi ya internet ya kudownload ya MB 3.5 kwa sekunde.

3. South Africa – South Africa inashika namba tatu kwa kuwa na kasi ya internet ya kudownload ya MB 4.36 kwa sekunde.

2. Morocco – Morocco inashika namba mbili kwa kuwa na kasi ya internet ya kudownload ya MB 4.38 kwa sekunde.

1. Kenya – Kenya imeshika nafasi ya kwanza kwa kuwa nchi yenye kasi ya internet ya kudownload ya MB 8.83 kwa sekunde. Kama unavyo ona Kenya ndio nchi yenye kasi kubwa kwa Afrika, sijajua kwanini Tanzania haikuwa kwenye utafiti huu lakini huwenda tukawa hatuko mbali sana na nchi ya Kenya. Pengine hii ndio sababu ya kenye kututangulia kwenye mambo mengi sana ya kiteknolojia ikiwa pamoja na hili la hivi karibuni la kufanikiwa kurusha Satelaiti yake ya Kwanza.

Tuambie maoni yako, unaonaje kuhusu list hii..? Unadhani Tanzania tutakuwa namba ngapi kwa nchi zenye kasi kubwa ya internet kwa Afrika..? Tuambie kwenye maoni hapo chini.

6 comments
  1. Very nice article. Ni kweli kabisa kuwa kasi ya internet huchangia kwa kiasi kikubwa manedeleo ya nchi husika

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use