Simu nyingi za sasa zinakuja na kioo ambacho ni full display huku sehemu za kuendeshea simu hiyo zikiwa kwenye kioo kwa chini. Sehemu hii kwenye simu za Android ndio huitwa Navigation bar.
Mara nyingi sehemu hizi huwa na rangi moja na huwezi kubadilisha sehemu hii mpaka utakapo fungua app ambayo inakuja na uwezo wa kubadilisha rangi ya sehemu hii. Mbali ya kubadilisha rangi pia huwezi kubadilisha muonekano wa sehemu hii zaidi ya kuchagua sehemu ambazo zipo kwenye settings pekee.
Kupitia makala hii nitakuonyesha njia bora ambayo unaweza kubadilisha rangi ya sehemu hii ya Navigation bar, ikiwa pamoja na kubadilisha muonekano wa sehemu hii kabisa. Bila kupoteza muda twende moja kwa moja kwenye makala hii.
Kwa kuanza download app kupitia link hapo chini, baada ya kudownload app kupitia link hapo chini endelea kwa kufuata maelekezo hapo chini.
Baada ya kuinstall app hiyo, moja kwa moja fungua app hiyo kisha bofya kitufe cha Let’s do it!’.
Baada ya hapo sasa moja kwa moja ruhusu app hii kwenye permission mbalimbali, bofya sehemu ya Allow App to draw over other apps.
Baada ya kuruhusu permission zote utapelekwa kwenye ukurasa wa nyumbani wa app hii, kisha moja kwa moja chagua sehemu ya ‘Active app’.
Pia unaweza kuchagua sehemu ya ‘Navigation Bar widget, sehemu hii itakusaidia kuweza kuonyesha picha mbalimbali kwenye sehemu hii ya Navigation. Pia unaweza kuchagua kuonyesha kiasi cha battery kilichopo kwenye simu yako kwa muda huo.
Pia unaweza kuwasha sehemu nyingine nyingi ambazo zipo ndani ya app hiyo na utaweza kuona sehemu ya Navigation ikiwa imebadilika.
Zipo app nyingine nyingi ambazo unaweza kutumia kubadilisha rangi ya navigation pamoja na sehemu mbalimbali kwenye sehemu ya Navigation bar kwenye simu yako. Apps hizo ni pamoja na zifuatazo.
App ya Stylish ni app nyingine ambayo inaweza kusaidia kubadilisha Navigation bar kwenye simu yako. App hii ni nzuri na kama unataka kubadilisha muonekano wa simu yako unaweza kutumia app hii pia, unaweza kudownload kupitia link hapo chini.
App nyingine ambayo inaweza kusaidia kubadilisha muonekano wa Navigation bar ni app hii ya Custom Navigation Bar, app hii ni rahisi kutumia na inaweza kusaidia kubadilisha muonekano wa simu yako kwa urahisi na haraka.
App nyingine ya Colorful Custom Navigation Bar inaweza pia kusaidia kubadilisha muonekano wa sehemu ya Navigation kwa urahisi na haraka, unaweza kupakua app hii pia kupitia link hapo chini.
Na hiyo ndio njia ambayo unaweza kutumia kubadilisha muonekano wa sehemu ya Navigation kwenye simu yako ya Android. Kama unataka kujifunza zaidi hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania tech, pia soma hapa kama unataka kubadilisha simu yako kuwa na muonekano wa simu mpya ya Galaxy S21.