Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

NASA Yagundua Sayari Saba Zenye Kuwezekana Kuishi Binadamu

Jiandae kufungasha kuelekea sayari nyingine
NASA Yagundua Sayari Saba Zenye Kuwezekana Kuishi Binadamu NASA Yagundua Sayari Saba Zenye Kuwezekana Kuishi Binadamu

Hapo jana shirika la NASA la nchini marekani lilitoa tangazo maalumu kuwa sasa kumepatikana sayari saba mpya, kwa mujubu wa NASA sayari hizo zenye ukubwa sawa na dunia zinauwezekano wa kuishi binadamu na kingine kizuri ni kuwa sayari hizo ziko karibu karibu sana.

Kikubwa na cha-kushangaza kuhusu uvumbuzi huu ni kuwa sayari hizo ziko karibu Karibu sana kiasi kwamba ukiwa kwenye sayari moja unauwezo wa kuona sayari nyingine zikipishana, pia vile vile sayari hizo ziko kwenye sehemu ambayo inawezekana kabisa sayari hizo kuwa na maji hivyo uwezekano wa viumbe hai kuishi huko ni mkubwa sana. Sayari hizo zimepewa jina la TRAPPIST kutokana na jina la darubini ambayo ndio ilitumika kugundua sayari hizo.

Advertisement

Kwa sasa habari pekee kuhusu ndani ya sayari hizo za TRAPPIST ni kuwa sayari hizo inaweza kuwa na barafu pekee uku zikizungukwa na maji mengi sana. Lakini bado watafiti hao hawajaingia ndani ya sayari hizo ila inategemewa kutengenezwa darubini mpya kutoka NASA ambayo ndio itasaidia kuangalia sayari hizo kwa nje pamoja na hali ya hewa ili kuhakiki kama sayari hizo zitafaa kuishi binadamu.

Kwa habari zaidi kuhusu sayari hizi unaweza kutembelea tovuti ya NASA kuangalia picha na video kuhusu sayari hizo. Hii ni habari kubwa sana kwa siku ya leo tarehe 23.02.2017 hivyo hakikisha unapitia tovuti hiyo ya NASA ili kujua zaidi kuhusu ugunduzi huo.

3 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use