Kwa sasa muundo na sifa za iPhone X, ni moja kati ya vitu vinavyo angaliwa sana na watu wengi pamoja na makampuni mbalimbali ya utengenezaji wa simu. Pengine kabla ya mwaka huu kuisha tarajia kuona simu nyingi sana ambazo zitakuwa ni nakala ya iPhone X.
Lakini kabla ya mwisho huo wa mwaka, tayari kampuni za nchini china zimeanza kutoa muundo wa simu hiyo ikiwa pamoja na kuongezea sifa zaidi tofauti na iPhone X yenyewe. Kampuni ya Doogee ya nchini china ndio ya kwanza kuja na simu hii ambayo kwa sura inafanana sana na iPhone X.
Kama unavyo ona kwenye picha hapo juu, tofauti iliyopo kwenye simu hiyo na simu halisi ya iPhone X ni kuwa simu hii ya Doogee V inakuja na sehemu ya Fingerprint kwenye kioo teknolojia ambayo ilitangazwa rasmi kwenye mkutano wa CES 2018, lakini sasa tayari inapatika kwa makampuni mengine mbalimbali.
Doogee V inategemewa kuzinduliwa tarehe 27 mwezi huu wa pili, huku ikiwa na kioo cha inch 6.2 kwa mujibu wa mvujishaji Evan Blass, mbali na kuwa na kioo kikubwa pamoja na mfumo wa uendeshaji wa Android 8.0, lakini ukweli ni kuwa bado simu hii ya Doogee V haita weza kukaribiana na teknolojia pamoja na mfumo mzima wa iPhone X.
Hii ni kutokana na teknolojia iliyotumika kwenye iPhone X ni ya bei ghali sana (ndio sababu ya simu hiyo kuuzwa ghali) na simu nyingi za nchini china zinategemewa kuuzwa kwa bei rahisi hivyo ni uhakika kuwa wanatumia teknolojia ya bei rahisi ambayo haiwezi kuwa sawa na teknolojia inayo tumiwa na Apple kwenye utengenezaji wa simu zake pamoja na iPhone X kwa ujumla.