Mobile World Congress ni mkutano mkubwa sana unaofanyika kila mwaka kuanzia mwezi wa pili kwenye mkutano huu makampuni mbalimbali ya simu hutumia wakati huu kuweza kutangaza bidhaa zao mpya kama matoleo mapya kwa mwaka huo, mkutano huo ufanyika nchini barcelona na haujawahi kufanyika nchi nyingine.
Baada ya kujua kwa ufupi kuhusu mkutano huo basi twende tukaangalie yote yatakayo jiri kwenye mkutano huo wa MWC wa mwaka huu 2017.
- LG MWC 2017
Kampuni ya LG imepanga kuwepo kwenye mkutano huo huku ikitegemewa kutangaza simu yake mpya ya LG G6 simu ambayo imekua gumzo sana kwenye mtandao siku za karibuni. Simu hii imapangwa kutangazwa hapo kesho tarehe 26 February huko nchini Barcelona.
- Samsung MWC 2017
Samsung imetangaza kuwa nayo itakuwepo kwenye mkutano huo, lakini bado habari hazija thibitisha kama Samsung itatangaza simu yake mpya ya Samsung Galaxy S8 kwenye mkutano huo. Baada yake kampuni hii ilitangaza kuzindua tablet yake mpya ya Samsung Galaxy Tab3. Tablet hii itazinduliwa hapo kesho tarehe 26 February kwenye mkutano huo wa MWC.
- Huawei/Honor MWC 2017
Huawei nayo haiko nyuma kwenye mkutano wa mwaka huu kampuni hiyo imepanga kutoa simu yake mpya ya Huawei P10 na Huawei P10 plus. Hawei imepanga kutangaza simu zake hizo mpya kesho tarehe 26 Febreary kwenye mkutano wa MWC huko nchini barcelona.
- TCL/BlackBerry MWC 2017
Kwa wapenzi wa blackberry leo siku ya tarehe 25 february kampuni hiyo kwa kushirikiana na kampuni ya TLC inatoa simu yake mpya ya Blackberry Mercury simu ambayo ilionekana awali kwenye mkutano wa CES wa mwaka 2017, tutakuletea habari kuhusu simu hii pale itakapo zinduliwa.
- HMD/Nokia MWC 2017
Kwa wapenzi wa siku nyingi wa Nokia ni muda sasa wa kupokea simu mpya kutoka kwa kampuni hiyo, Nokia imepanga kuwepo kwenye mkutano huo ili kuzindua baadh ya bidhaa zake ikiwepo Nokia 3310 pamoja na simu mpya za Nokia 6 pamoja na Simu zingine mpya zenye kutumoa android. Nokia inategemea kutangaza bidhaa zake hizo kuanzia kesho tarehe 26 February huko nchini Barcelona.
- Sony MWC 2017
Sony nayo imethibisha kuwepo kwenye mkutano huo, kam[puni hiyo imepanga kufanya uzinduzi wa simu zake mpya za Sony Xperia x2. Simu hizo zitazinduliwa kwenye mkutano huo kuanzia tarehe 29 February huko nchini Barcelona, kujua zaidi kuhusu simu hii endelea kutembelea Tanzania Tech.
- Alcatel MWC 2017
Kwa wapenzi wa simu za Alcatel kampuni hiyo imethibitsha kuwepo kwenye mkutano huo huku ikitegemewa kuzindua simu yake mpya ya Alcatel Idol 5 Pro, simu hiyo ambayo ilionyeshwa kwenye mkutano wa CES wa mwaka 2017 inategemewa kutangazwa tarehe 27 February kwenye mkutano huo wa MWC.
Na hayo ndio matukio makubwa ambayo yanasubiriwa kwenye mkutano huu mkubwa wa Mobile World Congress ambao umesha anza huko nchini Barcelona. Ili kujua mengine mengi endelea kutembelea Tanzania Tech kila siku kwani tutakuleta matukio yote jinsi itakavyokuwa. Pia usasahau kudowanload App ya Tanzania ili kukaa karibu na habari zote za teknolojia pindi zitakapo toka, kama unataka habari na maujanja kwa njia ya Video harakisha sasa jiunge na channel yetu ya Tanzania Tech kupitia mtandao wa Youtube.