Huu Ndio Mwanzo wa Teknolojia Nyingi Zilizo Badilisha Maisha

Huu ndio mwanzo wa mambo mbalimbali ya teknolojia
historia teknolojia historia teknolojia

Habari za jumapili mwana teknolojia, tunakutana tena mwisho wa wiki hii niki kuletea makala za je wajua tech kama kawaida ya siku za jumapili. Leo nimekuandalia mambo ambayo najua lazima utayapenda kwani nitaenda kukumbusha miaka flani ya nyuma jinsi teknolojia kadhaa zilipo anza na ilikuaje kwa kipindi hicho, basi bila kupoteza muda twende tukangalie mambo hayo.

  • USB Flash Drive ya Kwanza Kuingia Sokoni

Kwenye picha hapo juu hiyo ndio USB flash ya kwanza kabisa kuingia sokoni na flash hiyo ilitengenezwa na kampuni ya Israeli iliyokuwa inaitwa M-Systems. Flash hii ilikuwa na ukubwa wa MB 8 na ilianza kuuzwa rasmi mwaka 2000 na kampuni ya IBM.

Advertisement

  • Laptop ya Kwanza Kuingia Sokoni

Picha hiyo ni laptop ya kwanza ambayo ilikuwa inabebeka (portable computer) laptop hii iliingia sokoni April 3 mwaka 1981 na ilikuwa inaitwa Osborne 1. Laptop hii ilikuwa na uzito wa kilogram 10.7 kg na ilikuwa inauzwa na kampuni ya Osborne Computer Corporation kwa dollar za marekani $1,795.

  • Smartphone ya Kwanza Kabisa

Simu hii inasemekana ndio smartphone ya kwanza kabisa, simu hii ilitoka rasmi na kuingia sokoni August 16 mwaka 1994. Simu hii ilikua inauzwa na kampuni ya IBM na ilikuwa na ukubwa wa ndani wa MB 1 na uwezo wa RAM wa MB 1.

  • Simu ya Kwanza Yenye Kamera

J-SH04 ndio simu ya kwanza kabisa kuwa na kamera na simu hii ilitoka kwa jina la J-Phone chini ya kampuni ya Sharp. Simu hii ilitoka rasmi November 2000.

  • MP3 Player (MPman) ya Kwanza 

Kwa wale wahenga najua mtakua mnajua hii, Hii ni MPMan ambayo ndio Mp3 palyer ya kwanza kabisa, ilikuwa na uwezo wa MB 32 na ndio ya kwanza ambayo ulikua unaweza kuweka nyimbo zako mwenyewe.

Na hayo ndio mambo machache ambayo nimekuandalia siku ya leo kama una maoni maswali au ushauri usisite kutuandikia hapo chini kwenye sehemu ya maoni hadi jumapili ijayo nakutakia usiku mwema.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use