Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Jeshi la Polisi Limesema Mwanza Inaongoza Wizi wa Mtandaoni

Na dar es salaam nayo yatamba kwenye kwa matusi ya mtandaoni
Wizi mtandaoni Wizi mtandaoni

Pamoja na kuwa sheria za makosa ya mtandaoni lakini bado sehemu mbalimbali hapa nchini Tanzania zinaonekana kutofuata baadhi ya sheria hizo, hivi karibuni jeshi la polisi limetoa takwimu za makosa mbalimbali kupitia waandishi wa habari.

Katika Takwimu hizo mji wa dar es salaam umetajwa kuwa sasa unaongoza kwa kitendo cha kutukana au maneno ya kashfa kupitia mtandao, wakati jiji la mwanza likishika kinara kwenye wizi wa mtandaoni.

Advertisement

Takwimu hizo za Jeshi la Polisi zinaonyesha kuwa jumla ya matukio 327 ya matusi mtandaoni yameripotiwa kuanzia Januari hadi Juni mwaka 2017 jijini Dar es Salaam na wakati jumla ya matukio 1,663 ya wizi wa mtandaoni yakiripotiwa Mkoani Mwanza uku ukifuatiwa na Wilaya za dar es salaam za Ilala na Kinondoni.

Hata hivyo Msemaji wa jeshi hilo, Barnabas Mwakalukwa alisema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika ofisi za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA). alisema matukio mengi ya matumizi ya lugha za matusi mtandaoni yanatokea wilayani Temeke.

Mwakalukwa alisema kwa takwimu za mwaka jana, Arusha iliongoza kwa kuwa na matukio 312 ya mtandaoni ya kutishia kuua, ikifuatiwa na Kinondoni (295) na Mwanza (265). Kwa mwaka huu, watuhumiwa 315 walikamatwa kuanzia Januari hadi Juni kutokana na uhalifu wa mtandaoni na kesi 153 zimefunguliwa mahakama mbalimbali nchini Tanzania.

Takwimu hizo ni tofauti na za mwaka jana wakati watuhumiwa 1,080 walikamatwa kwa makosa ya uhalifu mtandaoni, huku kesi 578 zilifikishwa mahakamani na watuhumiwa katika 88 wakikutwa na hatia.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa Video.

Chanzo : Mwananchi

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use