Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Mwanamke Ajifunga Mwilini iPhone 102 Akitaka Kuzingiza China

Hii ndio njia ya iliyo kidhiri ya kuingiza simu nchini china kinyume na sheria
Mwanamke Ajifunga Mwilini iPhone 102 Akitaka Kuzingiza China Mwanamke Ajifunga Mwilini iPhone 102 Akitaka Kuzingiza China

Hivi karibuni kumekuwa na taarifa nyingi za watu mbalimbali kukamatwa na vitu vya ajabu sana kwenye sehemu za ukaguzi za uwanja wa ndege, lakini hii ni tofauti kidogo kwani hivi karibuni nchini china amekamatwa mwanamke aliyejifunga simu takribani 102 za iphone mwili mwake tayari kuzingiza China.

Mwanamke huyo ambaye aliji-funga simu hizo mwilini mwake kwa kutumia tepu na nguo maalum alikua akitoa simu hizo kutoka Hong-Kong na kuzingiza China. Unaweza kujiuliza kwanini mwanamke huyo aliamua kufanya hivyo, basi hii inasabishwa na simu hizo kuuzwa kwa bei rahisi sana Hong-Kong na kuuzwa bei ya ghali sana China.

Advertisement

Wakaguzi katika uwanja wa ndege wa Shenzhen Luohu nchini china wamesema walimuona mwanamke huyo akiwa amevaa nguo nzito sana za baridi wakati hiki ni kipindi cha joto ndipo walipo amua kumkagua na kumkuta na simu hizo pamoja na saa za mkononi vyote vilivyokuwa na uzito takribani pound 40 sawa na kilogram 19.

Hii sio tabia mpya nchini china kwani miaka iliyopita mtu mwingine mwanaume alikamatwa akiwa anataka kuingiza simu zaidi ya 146 za iPhone na ndio huyo ambaye mpaka sasa anashikilia rekodi ya kujifunga simu nyingi sana kwenye mwili wake.

Kwa habari zaidi za teknolojia endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

Chanzo : The Daily Dot, Kotaku

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use