Mwalimu wa kompyuta nchini Ghana Owura Kwadwo Hottish, ambae alikuwa gumzo kubwa kwenye mtandao wa Twitter siku za karibuni anaendelea kupata msaada zaidi kutoka kwa kampuni ya Microsoft Africa pamoja na wananchi wa nchini Ghana.
Hottish ambaye ni mwalimu wa kompyuta au (ICT) nchini Ghana, mwezi wa pili alikuwa gumzo baada ya kuchora kompyuta ubaoni kwaajili ya kufundisha wanafunzi kutokana na uhaba wa kompyuta shuleni hapo, kitendo ambacho kilimfanya apate umaarufu mkubwa pamoja na msaada wa kompyuta baada ya picha aliyo ituma kwenye mtandao wa Twitter kufikia mamilioni ya watu kwenye mtandao huo ikiwemo kampuni ya Microsoft Africa.
Hata hivyo mwalimu huyo ameendelea kupata msaada kutoka kwa kampuni ya Microsoft, hivi karibuni alionekana akiandika kwenye ukurasa wake wa Facebook kuwa yuko nchini Singapore alipo alikwa na Microsoft kwaajli ya kuudhuria mafunzo ya ziada kwenye mkutano wa Microsoft Global Education Exchange Summit unaofanyika kila mwaka. Mbali na hayo mwalimu huyo pia amekuwa akipokea misaada kutoka kwa kampuni hiyo pamoja na wananchi wa nchini Ghana.
Mwalimu Owura Kwadwo Hottish, ni moja kati ya mifano mingi inayo onyesha kuwa ukitumia teknolojia na mitandao ya kijamii vizuri unaweza kufika hata mahali ambapo ukuwaza kufika kiuchumi, kielimu hata kimaisha. Ni wakati sasa tuanze kutumia teknolojia kwenye maisha yetu ya kila siku huku tukizingatia sheria za mitandao.