Ni kweli kuwa wote tunapenda muziki iwe ni muziki wa kidunia au muziki wadini, lazima utakuwa unasikiliza muziki kwenye simu yako kwa namna moja ama nyingine. Sasa kuliona hili leo hapa Tanzania Tech tunakuleta app nzuri za kuwezesha kusikiliza muziki vizuri kwenye simu yako ya Android.
App hizi zinapatika kwenye soko la Play Store hivyo unaweza kudownload App hizi kupitia link chini ya jina la App husika. Basi bila kupoteza muda twende tukangalie App hizi nzuri.
1. AIMP
AIMP ni moja kati ya App nzuri sana za kusikiliza muziki, App hii haina mambo mengi lakini inakuja na uwezo mzuri wa kutoa sauti nzuri sana. App hii inapatikana Play Store na unaweza kuipakuwa kupitia link hapo juu.
2. JetAudio HD Music Player
JetAudio ni moja kati ya Player za siku nyingi sana, App hii ni nzuri na inakujlikana kwa kuwa na uwezo wa kucheza format mbalimbali za muziki. App hii inakuja na Equalizer zenye mfumo tofauti zaidi ya 10 ambazo zinaweza kukupa sauti nzuri sana unapo sikiliza muziki kwenye simu yako.
3. Rocket Music Player
Rocket Music Player ni application nyingine nzuri kwa ajili ya muziki kupitia simu yako ya Android, App hii inakupa zaidi ya Equalizer 10 ambazo zitakupa muziki mzuri sana. Pia unaweza kubadilisha muonekano wa app hii kwa kutumia Theme mbalimbali ndani ya App hiyo.
4. Phonograph Music Player
Kama wewe ni mmoja wa watu wanaopenda Player zenye muonekano mzuri basi app hii ni nzuri sana kwako. App hii inakupa muonekano mzuri sana na inauwezo wa mzuri wa kucheza muziki kwenye simu yako ya Android.
5. Pixel – Music Player
Kama simu yako inauwezo mdogo na ungependa kupata music player yenye uwezo mzuri basi hakikisha unapakua app hii. App hii inakuja na Equalizer 5 na inakuja na uwezo mzuri sana kwa kucheza muziki kwenye format za kawaida.
6. Impulse Music Player
Kama wewe ni kama mimi na ungependa kuwa na programu nzuri yenye uwezo mkubwa wa kucheza muziki kwenye simu yako basi hakikisha unajaribu app hii ya Impulse Music Player. App hii ni nzuri sana na ukweli nakushauri ujaribu kisha niambie kupitia maoni hapo chini.
7. Shuttle Music Player
Kama simu yako ni ya siku nyingi kidogo basi app hii ya muziki itakufaa sana, App hii inakuja na mfumo rahisi sana kutumia na inakupa aina 5 za equalizer kwa ajili ya kukupa aina tofauti za muziki kupitia simu yako ya Android.
8. BlackPlayer Music Player
Kama wewe unapenda muziki na unapenda kusilkiliza muziki wenye sauti nzuri basi jaribu app hii ya BlackPlayer Music Player. App hii inakupa aina tano za Equalizer na sehemu nyingine mbalimbali kwa ajili ya kufanya usikilize muziki vizuri.
9. PlayerPro Music Player (Free)
PlayerPro Music Player (Free) ni app nyingine ambayo mimi nitakushauri ujaribu kuitumia mia, app hii inakuja na uwezo mzuri sana na ukweli ni app nzuri sana na siwezi kuongelea app hii na kumaliza. Kitu cha msingi jaribu app hii kisha niambie kwenye maoni hapo chini.
Na hizo ndio app nzuri ambazio nimekuandali kwa siku ya leo, kama kuna app unayo ifahamu ambayo unahisi ni nzuri na ingetakiwa kuwa kwenye list hii basi tuambie kupitia sehemu ya maoni hapo chini. Kujua app nyingine nzuri unaweza kusoma makala yetu nyingine iliyopita, kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha unatembelea Tanzania Tech kila siku.