Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Muonekano wa TECNO Camon 20 Mr Doodle Edition

Simu ya Camon 20 yenye Doodles fahamu zaidi hapa
Muonekano wa TECNO Camon 20 Mr Doodle Edition Muonekano wa TECNO Camon 20 Mr Doodle Edition

TECNO CAMON 20, CAMON 20 Pro na CAMON 20 Premier ni matoleo mapya kwa mwaka huu wa 2023 kuachiliwa na kampuni ya simu za mkononi TECNO. Matoleo ya CAMON yamekuwa yakisifika katika ubora wa Camera na safari hii ukiiangalia vizuri CAMON 20 Series hasa hii mpya yenye kufahamika kama CAMON 20 series Mr Doodle edition utabaini ongezeko la ubunifu mpya katika Sanaa ya muundo ya mtindo wa simu hizi.

Muonekano wa TECNO Camon 20 Mr Doodle Edition

Advertisement

TECNO CAMON 20 premier doodle edition wakati wa usiku

TECNO ilianza na CAMON 20 series zenye jalada la Magic skin na sasa ni CAMON 20 yenye graffiti za Mr Doodle ambazo hung’aa kwenye jalada la simu hizi wakati wa siku.

Muonekano wa TECNO Camon 20 Mr Doodle Edition

TECNO imeshirikiana na mtu wa Sanaa Bwana Sam Cox almaarufu Mr Doodle katika kuleta Sanaa hii kwenye simu za CAMON 20.

CAMON 20 ya Doodle hufyonza mwanga wakati wa mchana na kuiachilia kama umeme wakati wa usiku, na hivyo kuruhusu sehemu ya nyuma ya simu kuonyesha kazi za graffiti za Mr Dooble. Muundo wa kipekee wa Toleo la Mfululizo wa CAMON 20 la Bw Dooble huifanya kuwa aikoni ya mitindo wakati wa mchana na kuvutia macho wakati wa usiku, na kuifanya kuwa bora kabisa inayochanganya mitindo na Sanaa na hii ndio tofauti kubwa kati ya TECNO CAMON 20 Mr Doodle na simu nyingine.

Muonekano wa TECNO Camon 20 Mr Doodle Edition

TECNO CAMON 20 Toleo la Dooble wakati wa mchana

Vile vile TECNO CAMON 20 Toleo la Dooble ina mandhari iliyogeuzwa kukufaa kwa mtindo wa grafiti ya Bw. Dooble, AR SHOT na AOD, kuleta mshangao zaidi kwa mtumiaji wakati wa uchukuaji picha.

TECNO CAMON 20 pro na TECNO CAMON 20 Premier zinaashiria maana halisi ya ubunifu na mabadiliko ya teknolojia kimuundo na kiutenda kazi, umahiri wa uchukuaji picha katika nyakati mbalimbali ni wenye ubora unaonekana kupitia picha na video za camera ya simu hizi.

TECNO CAMON 20 Pro 5G Dooble ina camera kuu ya Megapixel 64 nyuma (Night Potrait Master), 32MP Selfie Camera, 33W flash charge 5000mAh, 256GB ROM + 8GB RAM.

CAMON 20 Premiere 5G Doodle ina camera kuu ya Megapixel 108 wide angle (Night Portrait Master), 32MP Selfie Camera, 45W flash charge 5000mAh, 512GB ROM + 8GB RAM.

Kwa sasa CAMON 20 Mr Doodle edition zinapatikana kwa mkopo bila ya riba katika maduka yote ya simu nchini, Tembelea @tecnomobiletanzania au piga namba 0714029870 kwa huduma ya haraka.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use