Siku chache zilizopita kampuni ya Samsung ya nchini korea iliweka video ya tangazo la kioo cha simu cha aina ya Super Amoled. Ndani ya tangazo hilo inasemekana simu iliyotumiaka kuonyesha mfano wa kioo hicho ndio muonekano halisi wa simu mpya ya Samsung Galaxy S8.
Wataalamu wa mambo kupitia blog mbalimbali za teknolojia wanasema kuwa, hii ndio simu hiyo kutokana na kuwa simu hiyo iliyotumika kama mfano haina kibonyezo cha home botton na pia inaonekana kukaribia kutokua kabisa na bazel au upende wa plastic wa juu na chini.
Hata hivyo itakubidi usubirie mpaka mwezi, Aprili ili uweze kujua muonekano halisi wa simu hiyo kwa sababu kampuni hiyo imetangaza kusitisha kutoa simu yake hiyo mwezi February na kupeleka mpaka mwezi April mwaka huu.
Ili kujua zaidi kuhusu simu hii endelea kutembela Tanzania Tech au unaweza kupata habari kwa haraka kupitia App ya Tanzania Tech pamoja na Youtube Channel yetu.