Kama wewe ni mpenzi wa bidhaa za Apple najua utakuwa unajua kuhusu mkutano wa WWDC 2019, lakini kama ulikua hujui kuhusu hilo basi pengine ni wakati wa wewe kujua kuhusu ujio wa simu mpya za iPhone 11 na iPhone 11 Max.
Sasa ili kusudi uweze kuelewa zaidi labda tuanze nyuma kidogo kwenye mkutano wa WWDC 2019. Kwenye mkutano huo, Apple ilizindua mifumo yake ya iOS 13, macOS Catalina pamoja na kompyuta yake mpya ya Mac Pro. Hata hivyo kwenye uzinduzi huo kilicho chukua vichwa vya habari kwenye tovuti mbalimbali ni kioo cha kompyuta ya Mac Pro ambacho kilikuwa kinaitwa Pro Display XDR.
Kioo hicho kilikuwa kinauzwa takribani zaidi ya shilingi za kitanzania Milioni 10, Lakini hata hivyo kioo hicho haikuwa habari kubwa sana bali kilicho make headline kwenye kioo hicho ni stendi ya kuwekea kioo hicho. Stand hiyo ya kawaida, ilitangazwa kwenye mkutano huo ikiwa inauzwa kwa dollar za marekani $999, ambayo ni sawa na takribani shilingi za kitanzania Tsh 2,296,000 bila kodi.
Kama unavyoweza kuona picha hapo juu, stand hiyo ndio inauzwa Milioni 2.2 bei sawa na simu mpya ya Galaxy S10 Plus. Baada ya uzinduzi wa stand hiyo, mitandao mbalimbali ya kijamii ililipuka kwa vichekesho mbalimbali kuhusu stand hiyo huku wengi wakihoji nani ata nunua stand tu! kwa dollar za marekani $999.
Lakini kabla hili halijapoa, hivi karibuni kumekuwa na tetesi mbalimbali kuhusu picha ambazo zinasemekana kuonyesha muonekano wa simu mpya za iPhone 11 na iPhone 11 Max. Muonekano huo unaonekana kuchukiwa na watu wengi sana kutokana na mtindo wake wa kamera za nyuma.
Kama unavyoweza kuona kwenye picha hapo juu, simu hizo zinazo semekana kuwa ndio iPhone 11 na 11 Max, zinakuja na mtindo wa kamera tatu kubwa ambazo zimejipanga kwenye mpangilio ambao kwa namna moja ama nyingine unashangaza kidogo. Mbali na hayo kamera zote zipo kwenye sehemu ambayo inasemekana imetoka sana kwa mbele na kufanya simu hiyo kuonekana vibaya.
Mbali na hayo kwa mujibu wa tovuti ya Forbes, inasemekana kuwa simu hizo bado zitaendelea kuwa na ukingo wa juu maarufu kama Notch ukingo ambao unafanana na ule uliopo kwenye simu za iPhone XS na XS Max.
Sasa kwa kuwa wewe ni mpenzi wa simu za Apple, labda nikuulize swali.. Je unaonaje mtindo mpya wa simu za iPhone 11 na iPhone 11 Max..?. Binafsi yangu kweli muundo huu sioni kama ni muundo mzuri sana, pengine labda kuwe na sababu za kunishawishi, sababu zitakazo onyesha ubora wa kamera hizo ndio nikubali kuwa na simu zenye kamera kubwa zilizopo kwenye mtindo wa namna hiyo.
Kwako wewe hebu niambie kwenye maoni hapo chini… unaonaje muundo wa simu hizo mpya za iPhone 11 na iPhone 11 Max..? Je ungependa kuwa na simu yenye mtindo huo wa kamera…?
huo muonekano hauvutii bora wangezipanga kuelekea chini na hy sehm y kamera isingzid kwa mbele