Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Huu Ndio Muonekano wa Mfumo Mpya wa Uendeshaji wa Huawei

Inasemekana huu ndio muonekano wa awali wa mfumo wa Huawei
Huu Ndio Muonekano wa Mfumo Mpya wa Uendeshaji wa Huawei Huu Ndio Muonekano wa Mfumo Mpya wa Uendeshaji wa Huawei

Kama wewe ni mfuatiliaji wa maswala haya ya teknolojia basi najua unajua kuhusu katazo la kampuni za marekani kufanya biashara na kampuni ya Huawei, Katazo ambalo lilitolewa na serikali ya marekani na kusababisha kampuni nyingi za nchini humo ikiwa pamoja na Google kusitisha mfumo wa Android kwa kampuni ya Huawei.

Hata hivyo kutokana na hilo, kampuni ya Huawei hivi karibuni ilisemekana kuanza kufanya majaribio ya mfumo wake mpya ambao kwa sasa unajulikana kwa jina la HongMeng OS kwa nchini China na Ark OS kwa masoko mengine duniani kote.

Advertisement

Sasa ripoti mpya za hivi karibuni kutoka tovuti ya Phonearena zinasema kuwa, kampuni Huawei imeanza kuomba vibali vya kusajili mfumo huo kutoka kwenye nchi mbalimbali ili kuanza kutumia mfumo huo kwenye simu zake mpya zinazo tarajiwa kutoka karibuni. Mbali na hayo, Inasemekana mfumo huo kwa sasa upo kwenye hatua za mwisho za majaribio mara baada ya kujaribiwa na na kuonekana ukifanya kazi kwa haraka zaidi mara baada ya kujaribiwa na kampuni nyingine za simu kama Vivo, Oppo pamoja na Xiaomi.

Hata hivyo inasemekana kuwa mfumo huo umetengenezwa kwa ushirikiano wa kampuni ya Huawei, kampuni ya Tencent pamoja na kampuni za Oppo, Vivo na Xiaomi, zote zikiwa ni kampuni za nchini China.

Sasa katika hatua ya kuomba vibali vya kusajili mfumo huo, kume onekana screenshot ambazo zinasemekana kuwa ndio muonekano wa mfumo huo mpya ambao unategemewa kuja kwa awamu ya kwanza kwenye simu za Huawei zaidi ya milioni 1.

Huu Ndio Muonekano wa Mfumo Mpya wa Uendeshaji wa Huawei

Kama unavyoweza kuona hapo juu, hizo ni baadhi tu ya sehemu za mfumo huo ambao unasemekana utakuwa unafanya kazi kama mfumo wa Android ikiwa pamoja na uwezo wa kuinstall apps mbalimbali za sasa za Android. Picha nyingine za mfumo huo zinapatikana hapo chini.

 

Huu Ndio Muonekano wa Mfumo Mpya wa Uendeshaji wa Huawei

Huu Ndio Muonekano wa Mfumo Mpya wa Uendeshaji wa Huawei

Huu Ndio Muonekano wa Mfumo Mpya wa Uendeshaji wa Huawei

Huu Ndio Muonekano wa Mfumo Mpya wa Uendeshaji wa Huawei

Kama unavyoweza kuona picha hapo juu, Muonekano wa sasa wa mfumo wa HongMeng OS au Ark OS hauna tofauti sana na mfumo wa sasa wa EMUI 9. Hata hivyo bado hakuna ripoti kamili ya lini mfumo huu uta anza kutumika kwenye simu za Huawei, ila kama unataka kupata taarifa pale mfumo huu utakapo anza kutumika hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.

Kwa habari zaidi za teknolojia hakikisha unapakuwa app ya Tanzania Tech pia usisahau ku-subscriber kwenye channel YouTube channel yetu ya Tanzania Tech Hapa.

2 comments
  1. …kitu ambacho-sikielewi ni je katazo hilo la kibiashara kati ya makampuni ya Marekani na kampuni ya Huawei inahusu simu mpya zinazitajiawa kutoka tu au hataizi ambazo ziko mikononi mwa watumiaji?…

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use