Kampuni ya Samsung inategemea kuzindua simu zake mpya za Galaxy S20 pamoja na toleo jipya la simu mpya inayojikunja ambayo imepewa jina la Galaxy Z Flip, mwezi huu wa pili. Kama wewe ni mfuatiliaji wa tovuti ya Tanzania Tech na Price in Tanzania, basi lazima utakuwa umefanikiwa kuona sifa za awali za simu hizo ikiwa pamoja na muonekano unaotarajiwa kwenye simu hizo.
Lakini tofauti na hayo, hivi leo imesambaa video mpya mtandao ambayo ndio inasemekana ndio video ya kwanza inayoonyesha muonekano halisi wa simu mpya ya Galaxy Z Flip. Kwa mujibu wa tovuti ya The Verge, inasemekana video hiyo imevujishwa na Ben Geskin ambaye ni mmoja wa wavujishaji maarufu wanao tambulika kupitia mtandao wa Twitter.
Samsung Galaxy Z Flip – First Hands On Video pic.twitter.com/4b8Uzt5kRB
— Ben Geskin (@BenGeskin) February 2, 2020
Kama unavyoweza kuona kwenye video fupi hapo juu, Galaxy Z Flip inatarajia kuja na muundo unao fanana na ule wa simu inayo jikunja ya Motorola Razr ambayo imezinduliwa hivi karibuni lakini hadi sasa haija ingia sokoni.
Kwa upande wa Samsung Galaxy Z Flip, simu hiyo inasemekana itazinduliwa sambamba na Galaxy S20 lakini itachelewa kuwafikia watumiaji hadi mwezi wa tatu au wanne. Simu hiyo inasemekana kuja na kioo cha inch 6.7 ikiwa imefunuliwa, ukubwa wa ndani wa GB 128 au GB 256, RAM ya GB 8 pamoja na kamera tatu kwa ujumla.
Kama unataka kujua zaidi kuhusu simu hii hakikisha unaendelea kutembelea tovuti ya Tanzania Tech, pamoja na tovuti ya Price in Tanzania ambayo inakupa sifa na bei za simu mbalimbali kabla na baada ya kuzinduliwa rasmi.