Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Samsung Kuzindua Simu Mpya ya Samsung Galaxy J4 (2018)

Huu hapa ndio muonekano wa simu mpya ya Galaxy J4
Samsung Kuzindua Simu Mpya ya Samsung Galaxy J4 (2018) Samsung Kuzindua Simu Mpya ya Samsung Galaxy J4 (2018)

Kampuni ya Samsung iko njiani kuzindua simu zake mpya za Galaxy J Series, Simu hizi za bei rahisi tayari zimesha julikana kama ni simu za Samsung Galaxy J4 pamoja na Samsung Galaxy J6 zote zikitegemewa kuzinduliwa rasmi mwezi huu wa tano. Tayari tumesha ona muonekano wa Galaxy J6, na sasa twende tukaangalie muonekano wa Samsung Galaxy J4 (2018).

Samsung Galaxy J4 ni simu ambayo inategemewa kuwa na sifa za kawaida za simu nyingi za bei nafuu, pamoja na hayo Galaxy J4 inakuja na processor ya Exynos 7570 chipset ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 2 au RAM ya GB 3. Kwa upande wa ukubwa wa ndani utaweza kuchagua simu ya Galaxy J4 yenye ukubwa wa ndani wa GB 16 au GB 32.

Advertisement

Mbali na ukubwa wa ndani wa simu hii pia inakuja na kioo chenye ukubwa wa inch 5.5 chenye teknolojia ya Super AMOLED Display pamoja na Aspect ratio ya 16:9. Kamera ya nyuma ya simu hii inasemekana kuwa na uwezo wa Megapixel 13 huku ya mbele ikiwa na Megapixel 5, Battery ya simu hii inategemewa kuwa na uwezo wa 3000mAh ambayo itakuwa ni battery zile ambazo zinatoka. Kwa upande wa mfumo Galaxy J4 itakuja na mfumo wa Android Oreo 8.0 huku ikiwa na mfumo wa Samsung Experience 9.0.

Simu hii inategemea kuzinduliwa siku ya leo huku ikisemekana kuuzwa kwa dollar za marekani $200 ambayo ni sawa na Tsh 457,000. Kumbuka hii sio bei halisi zilizotangazwa hivyo endelea kutembelea Tanzania Tech kupata sifa kamili za simu hii pamoja na bei yake ambayo itatajwa na Samsung.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use