Ni wazi kuwa simu za Google pixel ni moja kati ya simu bora sana hasa kwenye upande wa kamera, simu hizi zimekuwa bora kuanzia toleo la kwanza la Google Pixel 1, hadi sasa toleo la Google Pixel 3 bado simu hizi zinaendelea kushika chati. Hivi karibuni Google Pixel 3 imekuwa kwenye chati mbalimbali za simu bora za mwaka 2018 na pia kwenye chati za simu zenye uwezo wa kamera nzuri kwa mwaka 2018.
Lakini ubora wa simu hizi haupatikani kwa bei rahisi kwani Google Pixel 3 na Google Pixel 3 XL zote zinapatikana kwa bei ghali kuanzia dollar za marekani $800 ambayo hii ni sawa na takribani shilingi za Tanzania Tsh 1,845,000 kwa toleo la kawaida la Pixel 3, ndio maana kampuni ya Google imejikita kuleta Google Pixel 3 Lite, toleo la bei rahisi la simu za Pixel 3.
Sasa tukiwa bado tupo kwenye chumba cha kusubiri, kwa mujibu wa tovuti ya The Verge, hivi karibuni muonekano wa simu hii umevuja rasmi na kuacha wapenzi wa simu hii wakiwa tayari wameshajua nini cha kutegemea kwenye simu hiyo mpya. Najua wewe pia unapenda kujua, ndio maana nami nakuletea yote muhimu unayo takiwa kujua kuhusu Google Pixel 3 Lite.
Kama umefanikiwa kuangalia Video hiyo hapo juu basi nadhani huna haja sana ya kuendelea kusoma, ila kama hujapata nafasi ya kuangalia video hii basi niruhusu nikueleze kidogo yaliyomo.
TABLE OF CONTENTS
Muundo
Kwa muundo inasemekana Google Pixel 3 Lite ina-fanana na Google Pixel 3 japokuwa Pixel 3 Lite yenyewe ni ndogo kwa ukubwa, simu hii inakuja na kioo cha LCD chenye ukubwa wa inch 5.56 chenye resolution ya 2220 x 1080. Pixel 3 Lite imetengenezwa kwa plastiki tofauti kabisa na toleo la kawaida la Pixel 3 ambayo imetengenezwa kwa chuma.
Kwa upande mwingine pia inasemekana Pixel 3 Lite inakuja na sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama headphone jack, tofauti na Pixel 3 na Pixel XL ambazo zote hazina sehemu hii. Kingine kuhusu muundo wa simu hii ni kuamishwa kwa tray ya kuweka laini ambayo sasa itakuwa inapatikana kwa pembeni na sio kwa juu. Vilevile simu hii itakuwa na kamera moja mbele na nyuma pamoja na spika moja kwa chini tofauti na matoleo ya Pixel 3 ambayo yanakuja na spika mbili.
Sifa za Google Pixel 3 Lite
Kwa upande wa sifa inasemekana Pixel 3 Lite inakuja na mfumo wa Android 9 (Pie), Processor ya Snapdragon 710 (10nm), GPU ya Adreno 615 pamoja na RAM ya GB 4 na ukubwa wa ndani wa GB 32. Kwa upande wa kamera Google Pixel 3 Lite inasemekana kuja na kamera ya Megapixel 12.2 kwa nyuma, na kamera ya Megapixel 8 kwa mbele kwa ajili ya kupiga picha za Selfie.
Mbali ya yote simu hii inasemekana kuendeshwa na battery yenye uwezo wa 2,915 mAh, battery ambayo ni sawa kabisa na ile ya kwenye toleo la Google Pixel 3 ya kawaida.
Mwisho kabisa inasemekana kama kama wewe ni “wazee wa instagram” au kama ulikuwa unasubiri simu hii kwa ajili ya kamera basi jiweke tayari kwani, inasemekana simu hiyo mpya ya Pixel 3 Lite inauwezo mzuri sana wa kupiga picha sawa kabisa na matoleo ya awali ya Google Pixel 3.
Inashauriwa kama ulikuwa unataka kununua Pixel 3 kwa ajili ya kamera, basi huna haja ya kuchezea pesa yako kwenye simu ya bei ghali, unachotakiwa kufanya ni kununua simu hii mpya ya Pixel 3 Lite ambayo inategemewa kutoka miezi michache ijayo.
That’s it guys, huo ndio muonekano wa simu mpya ya Google Pixel 3 Lite, Vipi umeonaje simu hii..? Ungependa simu hii iwe simu yako ya kuanza nayo mwaka mpya 2019, tuambie kwenye maoni hapo chini labda tunaweza kufanya kitu….!