Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Fahamu Yote ya Muhimu Kuhusu Samsung Galaxy Note 9

Haya ndio yote ya muhimu yaliyojiri kwenye mkutano wa uzinduzi wa Note 9
Fahamu Yote ya Muhimu Kuhusu Samsung Galaxy Note 9 Fahamu Yote ya Muhimu Kuhusu Samsung Galaxy Note 9

Kama wewe ni mfuatiliaji wa Tanzania tech na maswala ya teknolojia kwa ujumla najua jana ulifanikiwa kuona mubashara uzinduzi wa simu mpya ya Samsung Galaxy Note 9, Kama ukufuanikiwa kuangalia pia usijali kwani hapa nitaenda kukusanya yote ya muhimu unayotakiwa kujua kuhusu simu hiyo pamoja na uzinduzi huo kwa ujumla, kama unataka kujua sifa za Samsung Galaxy Note 9 unaweza kuangalia makala yetu iliyopita na utaweza kujua sifa za simu hii.

Kwa hapa tutaenda kuongelea yale ya muhimu ambayo kwa namna moja ama nyingine hatukuweza kupata nafasi ya kukwambia, sasa bila kupoteza muda let’s jump right in….

Advertisement

  • SPen

Kwa kuanza tukianza na SPen, kama wengi wenu mnavyojua hii ni kalamu maalum ambayo inakuja na simu za Galaxy Note kuanzia zililipo anza kutoka, Sasa tofauti na SPen za miaka ya nyuma sasa kalamu hii inakuja na teknolojia ya bluetooth, Kwa sasa bluetooth kwenye kalamu hii inauwezo wa kufanya mambo mbalimbali kama vile kufungua sehemu ya kamera na pia kupiga picha na kuitumia kama kiongozi cha wakati unafanya mkutano au (presentation) kwenye mkutano nadhani utaelewa zaidi ukinagalia video hapo chini.

Kwa sasa kitufe kwenye kalamu hii kinafanya mambo machache tuu huku ukiwa na uwezo wa kubadilisha matumizi ya kitufe hicho pale utakapo bofya mara moja, mara mbili au zaidi, mbali na hayo hiyo Samsung imesema inajiandaa kutoa programu kwa wabunifu wa programu ambao wataweza kubuni programu mbalimbali ambazo zitaweza kutumia kalamu hiyo. Na hiyo ndio SPen na yote ta muhimu unayotakiwa kuyajua.

  • Samsung DeX

Kwa wale wanaojua kuhusu simu za Galaxy Note 8 nadhani neno Samsung DeX sio geni sana. Samsung DeX ni aina mpya ya mfumo wa simu za Samsung ambao unakupa uwezo wa kutumia simu yako kupitia kioo cha kompyuta, mfumo huu unakuruhusu kuweza kutumia simu yako kama unavyotumia kompyuta yaani kwa kuunganisha Keyboard au kichapishio pamoja na Mouse au kibonyezeo cha kompyuta.

Sasa mwaka huu kupitia Galaxy Note 9, Samsung imeboresha zaidi mfumo huu ambao awali ili kutumia mfumo huu ulikua unachomeka simu yako kwenye kisahani maalum ndipo uweze kuwasha mfumo huo, kwa sasa samsung imeleta waya maalum ambao sasa utaweza kutumia ili kuunganisha kioo cha kompyuta yako pamoja na simu yako.

Mbali na hayo kama unataka pia utaweza kuendelea kutumuia simu yako kawaida kabisa bila matumizi yako kuonekana kwenye kioo cha kompyuta yako, yani utaweza kutumia simu na pia utaweza kutumia Samsung DeX kwenye kompyuta bila matumizi hayo kuingiliana pale unapokuwa umeunganisha simu yako.

  • Samsung Galaxy Watch

Mwaka huu pia samsung imetangaza kuleta saa zake za Galaxy Watch, saa hii itakuwa ni maalum kwa Note 9 na inakuja na kioo cha duara cha inch 1.3 ambacho kimetengenezwa kwa teknolojia ya Super AMOLED chenye resolution ya 360×360 pixel. Saa yenyewe imetengenezwa kwa chuma na mikanda yake imetengezwa kwa plastiki huku ikiwa na uwezo wa kubadilishwa kwa urahisi.

Saa hiyo inakuja na mfumo wa uendeshaji wa Tizen-based wearable OS 4.0, processor ya Dual-core 1.15 GHz yenye chipset ya Exynos 9110, Saa hii inakuja kwa aina mbili moja ikiwa ni LTE yenye ukubwa wa ndani wa GB 4 na RAM ya GB 1.5 na nyingine ya BBT yenye ukubwa wa ndani wa GB 4 pamoja na RAM ya MB 764. Saa hii inakuja na Teknolojia kadhaa kama vile teknolojia ya kutambua mapigo ya moyo, teknolojia ya kuzuia maji na vumbi pamoja na teknolojia ya kuchajiwa bila waya WPC wireless charging.

Battery ya Galaxy Watch ni battery isiyotoka yenye uwezo wa Li-Ion 472 mAh battery ambayo inasemekana inauwezo wa kudumu kwa muda wa siku nne kulingana na matumizi yako. Galaxy Watch inapatikana kwa Rangi nne za Silver (kwa saa kubwa ya 46mm); Midnight Black na Rose Gold (kwa saa ndogo ya 42mm). Kuhusu bei Galaxy Watch itauzwa kwa dollar za marekani $330 ambayo ni sawa na Tsh 754,000 bila kodi kwa saa ya 42mm, na Galaxy Watch ya 46mm itauzwa kwa dollar za marekani $350 sawa Tsh 799,000 bila kodi. Bei ni kwa mujibu wa viwango vya kubadilisha fedha vya siku ya leo hivyo bei inaweza kubadilika kwa Tanzania.

  • Galaxy Home

Kwa upande mwingine Samsung ilizindua spika zake maalum zinazotumia mfumo wa sauti wa Bixby ambapo unaweza kufanya mambo mbalimbali kama ilivyo kwenye spika za Google Home. Ikiwa ndio spika yao ya kwanza ya aina hii, Samsung imeshirikiana na kampuni ya AKG kutengeneza spika hiyo ambayo inakuja na MIC zaidi ya saba kwaajili ya kusikiliza chochote unachotaka kuambia ifanye ukiwa mahali popote.

  • Game ya Fortnite kwa Simu za Galaxy

Kitu cha mwisho ambacho ni muhimu kufahamu ni kuhusu game ya Fortnite, Game hii ni moja kati ya game maarufu sana na inachezwa na watu wengi sana duniani, kama tayari umeshajaribu game ya PABG basi lazima utaipenda zaidi game ya fortnite. Sasa kupitia mkutano uzinduzi wa Galaxy Note 9, Samsung kwa kushirikiana na kampuni ya utengenezaji wa Game hiyo inayoitwa Epic iltangaza kuwa game hiyo itaanza kupatikana rasmi kwenye mfumo wa Android na itapatikana kwa watumiaji wa simu za Galaxy kupitia soko la Galaxy Store.

Sasa kama ulikuwa hujui, kampuni ya Epic iliamua kutoweka game yake hiyo ya mfumo wa Android kwenye soko la Play Store kutokana na makato makubwa ambayo Google inayotaka kutokana na mapato ya Game hiyo. Hatimaye kampuni ya Epic iliamua kuachana na Play Store na kutangaza kuwa itakuwa inawezesha watu kudownload Game hiyo kupitia tovuti yake pekee na hapo jana watumiaji wa simu za Galaxy S7, Galaxy S7 edge, Galaxy S8+, Galaxy S8, Galaxy Note 8, Galaxy S9, Galaxy S9+, na Galaxy Note 9 ndio wataweza kupakua Game hiyo pekee kwa sasa kupitia soko la Galaxy Store.

Kama unatumia iPhone au iPad na unataka kujarib Game hii unaweza kubofya link hapo chini na utapelekwa kwenye soko la App Store kwaajili ya kupakua Game hiyo. Kama unatumia Android na unataka kujaribu kama Game hiyo inaweza kucheza kwenye simu yako, nimekuwekea link hapo chini pia unaweza kutumia link hiyo kupakua file ya APK na kujaribu kwenye simu yako.

Fortnite – iOS

‎Fortnite
Price: Free+

Fortnite – Android 

Download Hapa

So Far, hayo ndio yote ya muhimu unayotakiwa kujua kuhusu uzinduzi wa Samsung Galaxy Note 9, Kuhusu uchambuzi wa Galaxy Note 9 endelea kutembelea Tanzania Tech tunakuahidi tutakuletea yote ya muhimu ya kujua kabla hujafanya uamuzi wa kununua simu hiyo ya Galaxy Note 9.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use