Siku za karibuni kume ibuka utata mkubwa huko nchini china baada ya mtandao maarufu wa kuchat nchini humo WeChat kufanya mabadiliko ya sera za faragha na kuonyesha kuwa sasa data za siri za watumiaji wa mtandao huo zitaweza kuonekana na serikali ya China.
Utata huo ambao ulianza toka juzi, sasa umefikia kwenye hatua ya aina yake baada ya serikali ya nchini humo kuamua kufungia mtandao wa WhatsApp nchini humo, aidha inasemekana kuwa China imefanikiwa kutengeneza programu maalum ya kuweza kuangalia data hizo za siri kwenye mitandao kama ya WeChat lakini ugumu ulikuja kwenye mtandao wa WhatsApp sababu ya sehemu ya programu hiyo kuwa na ulinzi zaidi ndipo serikali ya nchi hiyo ilipo amua kupiga marufuku programu hiyo kutumika nchini humo.
Hata hivyo data ambazo serikali ya China inaweza kuziona moja kwa moja kutoka programu mtandao wa WeChat ni kama vile, majina ya watu kwenye programu hiyo, Namba za simu, Barua pepe pamoja na mahali ulipo kupitia Google Maps.
Hata hivyo kwa wale ambao mlikua hamjui WeChat ndio mtandao maarufu zaidi wa kuchat nchini China ukiwa na idadi ya watumiaji zaidi ya milioni 600 huku ukiwa ndio mtandao unaotumika zaidi nchini china zaidi ya Facebook na WhatsApp.
Mtandao wa WeChat unatumika hata nje ya china na unaweza kudownload kupitia Google Play, lakini ni vyema kutokutumia mtandao huo kwa sasa kutokana na kutokuwa na ufaragha.
Kupata habari zaidi kuhusu sakata hili, endelea kutembelea Tanzania Tech pia unaweza kudownload App ya Tanzania Tech ili kupata habari zote za teknolojia kwa haraka, pia usisahu kujiunga na channel yetu ya Tanzania Tech ili kupata habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia kwa Video.
Chanzo : The Epoch Times