Kama wewe ni msomaji wa tovuti ya Tanzania tech basi najua unajua kuwa tulisha wahi kuongelea mada kama hii ya jinsi ya kubadilisha muandiko kwenye simu mbalimbali ikiwa pamoja na simu za Tecno. Lakini kama wewe ni mmoja wa watu wanaotumia simu za Tecno au Infinix na umeshindwa kuweka miandiko mipya kwenye simu yako basi makala hii ni kwa ajili yako.
Kitu cha msingi unachotakiwa kujua ni kuwa hii sio makala ya jinsi ya kubadilisha muandiko kwenye simu yako bali hii ni makala ya jinsi ya kuongeza miandiko ya ziada kwenye simu yako ya TECNO au Infinix. Kama unataka kujifunza jinsi ya kubadilisha muandiko kwenye simu za Tecno unaweza kusoma hapa na fuata hatua kwa hatua.
Basi baada ya kusema hayo basi moja kwa moja twende kwenye hatua jinsi ya kuongeza miandiko mbalimbali kwenye simu yako. Hatua ya kwanza unatakiwa kupakua app inaitwa Magic Font (2019), unaweza kupakua kupitia link hapo chini.
Baada ya kupakua app hiyo na kuinstall vizuri kwenye simu yako basi moja kwa moja fungua app hiyo kisha bofya sehemu iliyo andikwa Font. Kisha baada ya hapo chakua muandiko unao hitaji kisha endelea kwa kubofya sehemu ya Download.
Baada ya kumaliza hatua zote hizo malizia kwa kubofya kitufe cha OK pale unapo maliza kudownload muandiko wako kupitia app hii. Kwa kubofya hapo basi utakuwa umeongeza muandiko mpya kwenye simu yako ya Tecno au Infinix.
Kwa sasa app hii imeonekana kufanya kazi kwa asilimia kubwa kwenye simu za Tecno au Infinix, binafsi nimejaribu kwenye Galaxy S9 pamoja na Galaxy C7 zote zimeonekana app hii kutofanya kazi vizuri, hivyo kama unatumia simu za samsung basi fuata njia nilizo kuelekeza kwenye post hapa.