Mtandao wa kijamii uliokuwa unajulikana kama Twitter sasa umekuwa rasmi X.com kwenye mifumo yake yote ya msingi. Hii inamaanisha kwamba ukiandika twitter.com kwenye kivinjari chako, utapelekwa kwenye tovuti inayopendekezwa na Elon Musk, ambayo ni X.com
Kwa sasa Ujumbe unaonekana chini ya ukurasa wa kuingia wa X ukisema, “Tunakuarifu kuwa tunabadilisha URL yetu, lakini mipangilio yako ya faragha na ulinzi wa data inabaki kuwa kama kawaida.”
All core systems are now on https://t.co/bOUOek5Cvy pic.twitter.com/cwWu3h2vzr
— Elon Musk (@elonmusk) May 17, 2024
Mabadiliko ya jina la tovuti yamekuwa moja ya vipengele vigumu vya hatua ya Elon Musk kubadilisha jina la kampuni. Ingawa vipengele vingi vya X vilihamia kwenye chapa mpya muda mrefu uliopita — ikijumuisha akaunti rasmi, programu za simu, na “X Premium” (zamani Blue) — URL za akaunti za watumiaji zilibaki kuwa twitter.com tangu Musk alipoanzisha rasmi mabadiliko hayo.
URL zilianza kubadilika tangu Agosti mwaka jana, wakati baadhi ya watumiaji waliweza kunakili viungo vya x.com kutoka kwa programu ya X ya iOS.
Musk ana historia ndefu na URL au tovuti ya x.com, mwazo Musk alizindua biashara chini ya jina hilo mwaka 1999 ambayo hatimaye iliungana na kile kilichokuwa PayPal. Kwa sasa Elon Musk anatarajia toleo hili la X.com itakuwa programu jumuishi ambayo itafanana utendaji kama WeChat ya nchini China.