Hadi sasa ni mambo mengi sana yanaendelea kuhusu mtandao wa TikTok, hivi karibuni mtandao huo ulipigwa marufuku nchini India ikiwa pamoja na apps nyingine 58 ambazo zinasemekana kuwa zimetengenezwa na kampuni za kichina.
Lakini kama haitoshi, huko HongKong nako kampuni ya TikTok imesitisha huduma zake kutokana na sheria kali za serikali.
Kama hayo yote hayatoshi, hivi karibuni Raisi wa Marekani ametangaza kuifungia app ya TikTok kutotumika nchini Marekani.
Yote haya yamekuja mda mchache baada ya taarifa kusambaa mtandao zikisema kuwa kampuni ya Microsoft ipo kwenye maongezi na kampuni ya Byte Dance ambayo ndio miliki wa mtandao wa TikTok kwa nia ya kununua mtandao huo.
“Nitasaini hati hiyo kesho,” Trump alisema maneno hayo kwa waandishi wa habari Ijumaa usiku, na kuashiria kwamba marufuku hiyo inaweza kuanza “hivi karibuni (Jumamosi ya leo)”.
Bado haija eleweka wazi ni kwa jinsi gani utawala wa Trump utalazimisha marufuku ya TikTok nchini Marekani, ingawa kuna njia za tofauti za kuzuia mtandao kama vile kutumia Firewall, ingawa njia hizo hazijawahi kufanywa au kutumika huko nchini Marekani.
Inaelezwa kuwa, sheria za Marekani hazina mfano wowote wa kuzuia programu kwa njia hiyo, hivyo hakuna uwezekano kama marekani itaweza kuzuia mara moja mtandao wa TikTok ndani ya siku ya leo au hivi karibuni.
Hata hivyo baada ya Raisi Trump kutoa kauli hiyo, Meneja Mkuu wa mtandao wa TikTok nchini Marekani Vanessa Pappas, amejibu kwa njia ya video huku akisema “Hatuna mpango wa kwenda popote.” Kampuni hiyo italeta ajira 10,000 nchini Merika kwa miaka mitatu ijayo, Tuko hapa kwa muda mrefu.” alisema Pappas.
@tiktok A message to the TikTok community.
Kwa sasa baadhi ya watumiaji maarufu wa mtandao wa TikTok wa nchini marekani wameanza kutangaza kwa wafuasi wao kuwafuata kwenye mitandao mingine ya kijamii, huku ikisemekana na kutokana na kauli hiyo ya raisi wa marekani ya kufungia mtandao wa TikTok hivi karibuni.