Dunia ya mitandao ya kijamii inazidi kuleta mabadiliko na uvumbuzi mpya kila siku. Habari njema kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii wanaopenda kushiriki na kuunganika na marafiki zao na jamii kwa njia ya pekee. Huduma maarufu ya mtandao wa kijamii “Threads,” iliyokuwa inapatikana kupitia apps sasa inapatikana kupitia tovuti.
Threads, ambayo awali ilikuwa inapatikana kwenye mfumo wa Android na iOS pekee sasa inaweza kutumiwa na mtu yoyote kupitia kifaa chochote kinachotumia browser au Kisakuzi.
Mtumiaji wa Threads sasa hana haja ya kuwa na app ili kutumia mtandao huo wa kijamii, bali unahitaji kutembelea tovuti ya Threads ambayo ni Threads.net
Unachotakiwa kufanya unapofika kwenye ukurasa huo ni kuingiza password na username ambayo unatumia kwenye akaunti yako ya Instagram iliyo unganshwa na akaunti ya Threads.
Threads.net inaleta utendaji sawa na programu za simu, ikiwa pamoja na uwezo wa kuandika maandishi, kupost link, kuongeza picha, video, na maandishi kwenye post yoyote. Kwa sasa unaweza kutufuata kwenye mtandao wa Threads kupitia threads.net@tanzaniatech_