Kwa mujibu wa tovuti ya The Citizen, Hivi karibuni kampuni ya Azam inategemea kuja na mtandao wake wa simu ambao utajikita kutoa huduma za gharama nafuu hapa nchini Tanzania. Kwa mujibu wa habari hizo, mtandao huo wa simu utakuwa ukiitwa Azam Telecom huku jina la kibiashara la mtandao huo likiwa ni Azam Telecom (T) Limited, kampuni ambayo itakuwa chini ya kampuni ya Bakhresa Group of Companies.
Kwa mujibu wa The Citizen, ambayo ilifanya mahojiano na Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa kampuni ya Bakhresa Group, Hussein Sufian Ally, tayari kampuni hiyo imeshapata baadhi ya vibali muhimu kutoka TCRA vibali vitakavyo iwezesha kampuni hiyo kujenga mnara ambao utawezesha Azam Telecommunications kutoa huduma ya kasi ya mtandao huduma inayo julikana kama 4G miongoni mwa huduma za kawaida za Mawasiliano.
Bado hakuna taarifa kamili lini huduma hizi zita anza kutolewa rasmi na mtandao huo mpya wa simu, ila kwa mujibu wa The Citizen, huwenda Azam Telecom ika anza kutoa huduma zake kwenye miezi ya karibuni. Endelea kutembelea Tanzania Tech kujua zaidi.
Ongera sana naona mtandao huu utakua kimbilio la watanzania