Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Mtandao wa Internet Wafikisha Miaka 30 Toka Kuanzishwa Kwake

Mtandao au World Wide Web ulizaliwa rasmi siku kama ya leo
Mtandao wa Internet Wafikisha Miaka 30 Toka Kuanzishwa Kwake Mtandao wa Internet Wafikisha Miaka 30 Toka Kuanzishwa Kwake

Kama ulikiuwa hujui basi leo ni siku muhimu sana kwetu watumiaji wa mitandao mbalimbali kote duniani kwani, bila siku kama ya leo basi wote tusingekwepo hapa tukijadiliana na kupeana habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia. Siku kama ya leo tarehe 12 March ndipo mtandao wa internet au World Wide Web ulipozaliwa.

Sasa tukija kwenye upande wa historia, Mtandao wa internet uligunduliwa mwaka 1989 na Sir Tim Berners-Lee ambaye alikuwa akitaka kurahisisha mawasiliano kati ya watafiti wa kisayansi ili kuweza kurahisha kushirikiana matokeo ya data za utafiti wao kwa urahisi na haraka. Kwa kipindi hicho internet ilikwepo lakini kulikuwa hakuna mtu aliyefikiria kama kuna uwezekano wa ku-unganisha document moja na nyingine kupitia internet.

Advertisement

Mtandao wa Internet Wafikisha Miaka 30 Toka Kuanzishwa Kwake

Kwa mujibu wa tovuti ya Google arts and culture, Berners-Lee aligundua mtandao wa internet au World Wide Web akiwa anafanya kazi kwenye kituo cha Shirika la Ulaya la Utafiti wa Nyuklia nchini Uswisi CERN. Hata hivyo inasemekana wazo la Berners-Lee lilikuwa zaidi ya kuwezesha mawasiliano kwa watafiti wa kisayansi na baada ya muda mchache ubunifu wake uliwezesha mawasiliano kwa watu wote duniani.

Baada ya muda kidogo watu na kampuni mbalimbali zilianza kutengeneza tovuti mbalimbali, unaweza kuangalia video hapo chini kujua zaidi kwa undani zaidi.

Hadi sasa kuna mitandao mingi sana inayotumika kutoa taarifa na kuunganisha ndugu, jamaa na marafiki, ni muhimu kusherekea siku hii kwani hata hivyo baada ya kuanzishwa kwa Internet tarehe 12 March. Tarehe 13 March 2016 ndipo mtandao wa Tanzania Tech ulipo zaliwa rasmi.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use