Google Yatangaza Kusitisha Huduma za Tovuti ya Google+

Mtandao huo utafugwa rasmi baada ya miezi 10
mtandao wa Google+ wasitishwa mtandao wa Google+ wasitishwa

Mtandao wa Google+ ulianzishwa mwaka 2011 kama moja ya mtandao wa kijamii ambao unamilikiwa na kampuni ya Google, Mtandao huo ulikuwa na kuongezeka umaarufu kipindi cha mwanzoni wakati mtandao huo ulipo zinduliwa lakini kadri miaka ilivyozidi kwenda mtandao huo ulipoteza umaarufu kutokana na mitandao mingine ya kijamii kama Facebook kupata umaarufu.

Kwa kipindi kirefu mtandao wa Google+ umekuwa ukifanya vibaya kutoka na kutokuwa na watumiaji wa kutosha pia umekuwa ni mtandao usiojulikana na watu wengi japokuwa app ya mtandao huo ilikuwa ikiwekwa kwenye simu nyingi zinazotumia mfumo wa Android.

Advertisement

Sasa baada ya kuliona hilo hapo jana kampuni ya Google kupitia blog yake iliandika makala kuhusu matarajio ya kufunga mtandao huo hasa kwa upande wa watumiaji wa kawaida. Google kupitia ukurasa huo imeandika kuwa imefikia hatua hiyo baada ya udhaifu wa usalama uliotangulia ambao ulisababisha data za wasifu za watumiaji kuvuja hapo mwezi Machi 2018.

Hata hivyo kampuni ya Google imeandika kuwa toleo la mtandao huo kwaajili ya makampuni litaendelea kuwepo kama kawaida ila toleo la watumiaji wengine wa kawaida ndilo litakalo sitishwa baada ya miezi 10 kutokea hivi leo. Mbali na hayo google imefanya mabadiliko mengine kwenye upande wa wabunifu wa programu kwa kuweka baadhi ya vikwanzo kwenye mfumo wa API, unaweza kusoma mabadiliko hayo hapa.

Google imeandika kuwa mabadiliko hayo yanakuja kama sehemu ya mabadiliko ambayo yamepewa jina la Project Strobe ambayo inahusisha mabadiliko dhidi ya wabunifu wa programu mbalimbali wanaotumia mfumo wa Google API kwenye mfumo wa android na mifumo mingine. Kwa sasa Google imetangaza kuwa bado inafanyia kazi njia mpya ya kuwezesha watumiaji wa mtandao huo kupakua data zao kutoka kwenye mtandao huo wa Google+.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use