Follow

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use
English

Tovuti Zinazoweza Kukusaidia kupata Msaada wa Kifedha

Unaweza kupata msaada wa kifedha wa jambo lolote unalotaka kufanya
Tovuti Zinazoweza Kukusaidia kupata Msaada wa Kifedha Tovuti Zinazoweza Kukusaidia kupata Msaada wa Kifedha

Ni wazi kuwa kila mmoja wetu hajajitosheleza na kuna wakati unapitia magumu kiasi kwamba unatamani kuomba msaada kwa jamii kwa sababu ya kushindwa kabisa kutoka kwenye hali uliyopo.

Kama wewe ni mmoja wa watu wanao pitia hali ngumu ya maisha kwa sasa basi usikate tamaa kwani makala hii inaweza kukusaidia kwa namna moja ama nyingine.

Advertisement

Kupitia makala hii tutaenda kuangalia tovuti bora ambazo zinaweza kukusaidia kupata msaada wa kifedha ili kuweza kutoka kwenye tatizo ulilonalo, kumbuka hata wewe ambae kwa sasa upo kwenye furaha unaweza kushirikiana na mwenzako kugawana furaha hiyo kwa kumsaidia kwa hali na mali, basi baada ya kusema hayo twende moja kwa moja kwenye makala hii.

Gofundme

Tovuti Zinazoweza Kukusaidia kupata Msaada wa Kifedha

Gofundme ni tovuti bora ambayo inaweza kukusaidia kupata msaada wa kifedha, kama wewe ni mtu mwenye tatizo la kiafya na unahitaji matibabu au kama unataka kufanya jambo kwa ajili ya watu wengine au kama unataka kujiendeleza na umeshindwa kulipia baadhi ya ada, au kama unataka kuanzisha kampuni yenye kutoa msaada kwa jamii basi tovuti hii ni nzuri kwako.

Unaweza kutengeneza ukurasa bure kupitia tovuti hiyo, kisha elezea story yako weka picha na video zenye kuonyesha tatizo lako kwa undani kisha weka kiwango cha pesa unacho hitaji kuondoa tatizo lako alafu post ukurasa wako.

Kupitia tovuti hiyo watu kutoka nchi mbalimbali watakuchangia hadi kufikia lengo lako ili kuondoa tatizo lako. Baada ya lengo lako la kifedha kutumia utaweza kutoa pesa zako kuingia kwenye akaunti yako moja kwa moja.

Tembelea Tovuti Hapa

Gogetfunding

Tovuti Zinazoweza Kukusaidia kupata Msaada wa Kifedha

Kama ilivyo tovuti iliyo tangulia, Gogetfunding ni tovuti nyingine ambayo itakusaidia sana kupata msaada wa kifedha, jinsi ya kutumia tovuti hii ni kama ilivyo tovuti iliyo tangulia. Unatakiwa kutengeneza ukurasa wa bure uku ukielezea tatizo lako kwa video na picha, kisha weka kiwango unachotaka ambacho kitatatua tatizo lako alafu post ukurasa huo.

Watu wataweza kukupa msaada hadi kufikia lengo lako na baada ya hapo utatuma pesa zako kwenye akaunti yako. Kumbuka unaweza kutumia tovuti hii kwa msaada wowote wa kifedha kitu cha muhimu ujue jinsi ya kujieleza vizuri kwa kutumia lugha ya kingereza.

Tembelea Tovuti Hapa

Crowdrise

Tovuti Zinazoweza Kukusaidia kupata Msaada wa Kifedha

Crowdrise ni tovuti nyingine ambayo inaweza kukusaidia kupata msaada wa kifedha, tofauti ya tovuti hii na nyingine zilizopo kwenye list hii ni kuwa tovuti hii ni kwa ajili ya taasisi zisizo za kifedha. Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wana andaa matamasha kwa ajili ya jamii basi unaweza kupata fedha za kuandaa tamasha hilo kupitia tovuti hii.

Kama ilivyo tovuti zilizotangulia, unaweza kutengeneza kurasa kuhusu na tamasha lako, kisha weka sababu ya kufanya tamasha lako pamoja na picha au video kisha weka kiasi cha fedha unachohitaji alafu malizia kwa kupost ukurasa huo.

Tembelea Tovuti Hapa

Na hizo ndio tovuti ambazo ni uhakika kuweza kupata msaada wa kifedha kwa urahisi, unacho takiwa kujua ni kuwa baadhi ya tovuti hizi zinachukua asilimia kadhaa ya pesa ulizo changiwa, hii inasaidia kwa tovuti hizo kuendelea kuwepo mtandaoni na kutoa msaada kwa watu wenye uhitaji.

Kumbuka usitumie tovuti hizi vibaya kwani kufanya hivyo utafungiwa kutumia tovuti hizo au ukurasa wako kufutwa kabisa kwenye tovuti hiyo, pia ili kufanikiwa hakikisha una andika ukurasa wenye tija uki ambatanisha na picha au video za tatizo lako.

5 comments
  1. Kwa jina naitwa ramson samweli kutoka morogoro nilikua naomba mnikopee pesa kama sh.50000 iv niogezee mtaji minafanya biashala ya unadishaj wa nguo

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use